Search the region
22813 stories
PSSSF :TUTALINDA HAKI NA MASLAHI YA WANACHAMA
Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi, akifungua semina ya mafunzo kwa waajiri kutoka Taasisi na Halmashauri za Mkoa wa Dodoma kuhusu majukumu na Huduma zitolewazo na PSSSF Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifiatilia hotuba na mawasilisho mbalimbali ya mada l Dodoma, Oktoba 6, 2026 Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umeahidi kulinda haki na maslahi ya wanachama wake, kurahisisha huduma na kudumisha mahusiano na mawasiliano ya wazi na Waajiri kote nchini. Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Paul Kijazi wakati akifungua semina iliyohudhuriwa na waajiri 462 wa kanda ya kati iliyofanyika Oktoba 6, 2026, Makao Makuu ya PSSSF jijini Dodoma. Semina hiyo ililenga kujenga uelewa wa pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Mfuko na Waajiri ili kurahisisha utatuzi wa changamoto za wanachama na kuboresha utoaji wa huduma. Semina hiyo iliyohudhuriwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Hajji Khamis na Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw. Sayi Lulyalya, Bw.Kijazi alisisitiza umuhimu wa Waajiri kutimiza wajibu wao kwa wakati na kutumia mifumo ya kidigitali ili kulinda haki na maslahi ya watumishi kwa lengo la kuharakisha huduma. “Hatua za kuimarisha mifumo ya kidigitali na ushirikiano wa karibu zinatarajiwa kuondoa ucheleweshaji wa malipo ya mafao, kuhakikisha taarifa za wanachama zinahuishwa mara kwa mara, na kuongeza ufanisi wa jumla katika utoaji wa huduma zetu” alifafanua Bw. Kijazi Katika semina hiyo, mada mbalimbali ziliwasilishwa na kujadiliwa ikiwemo; matumizi ya Mfumo wa PSSSF Member Portal, Uwasilishaji wa Nyaraka za Madai ya Mafao, na Taratibu za Usajili wa Watumishi wapya.</
Wed, 07 Oct 2026 16:06:32 +0000Uganda Calls for Regional Push to Scale Locally Led Climate Adaptation
Read the full report from the original source.
RecentlyMEYA KIBAHA ATOA SIKU SABA KWA KIWANDA CHA CORDY KUKOMESHA UTIRIRISHAJI WA MAJI MACHAFU
Na Victor Masangu, Kibaha MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Dkt. Mawazo Nicas, ametoa siku saba kwa kiwanda cha kuchakata plastiki cha Cordy, kilichopo Kata ya Picha ya Ndege, kuhakikisha kinaweka mfumo sahihi wa majitaka na kuacha kutiririsha maji machafu katika maeneo ya makazi ya wananchi. Dkt. Nicas ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda hicho na kubaini kuwa bado kinaendelea kutiririsha maji machafu katika maeneo yanayozunguka makazi ya wananchi, licha ya kupewa maelekezo mara kadhaa na viongozi mbalimbali. Ziara hiyo imefanyika kufuatia malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi wa Mtaa wa Picha ya Ndege kuhusu harufu kali pamoja na maji yenye rangi nyeusi yanayotiririka mitaani na kuingia katika makazi yao. Wananchi wamedai kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha athari mbalimbali kwa jamii na viumbe hai, ikiwemo mifugo kufa baada ya kunywa maji hayo. Akiwa katika eneo hilo, Dkt. Nicas akiwa na timu kutoka Idara ya Mazingira ya Manispaa, alibaini kuwepo kwa bomba pamoja na chemba iliyokuwa imeelekezwa moja kwa moja kwenye mtaro unaopita katika maeneo ya makazi ya wananchi. Dkt. Nicas amesema Manispaa hiyo imewahi kufika katika kiwanda hicho na kutoa maelekezo ya kukomesha tatizo hilo, lakini utekelezaji wake haujawa wa kuridhisha. Amesema kiwanda hicho hakina mfumo wa kutibu na kuchuja maji taka kabla ya kuyatoa nje ya kiwanda, huku pia kikiwa hakina kibali kutoka mamlaka husika ya Bonde la Maji kwa ajili ya kutiririsha maji. “Tumeshafika hapa mara ya kwanza na kutoa maelekezo, lakini wamekuwa wakaidi. Hili ni jambo hatari kwa afya ya jamii,” amesema Dkt. Nicas. Ameagiza kiwanda hicho ndani ya siku saba kujenga mfumo wa kutibu maji taka kabla ya kuyatiririsha, huku mamlaka ya bonde ikitakiwa kufanya taratibu za ukaguzi na utoaji wa kibali baada ya maji hayo kutibiwa kwa mujibu wa taratibu. Aidha, Dkt. Nicas ametoa muda hadi Jumapili, Oktoba 12, 2026, kwa kiwanda hicho kuhakikisha kinavisafisha vyanzo na mtaro unaopokea maji hayo machafu. Amesema atarejea katika eneo hilo kukagua utekelezaji wa maagizo hayo na kwamba iwapo hayatatekelezwa, Manispaa itachukua hatua kwa mujibu wa sheria. Kwa upande wake, Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Bryson Mpogoza, amesema kiwanda hicho kiliwahi kutozwa faini na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), baada ya kubainika kutotekeleza matakwa ya kimazingira. Amesema kiwanda hicho kiliahidi kutekeleza maelekezo yaliyotolewa, lakini ukaguzi wa hivi karibuni umebaini kuwa baadhi ya changamoto bado zinaendelea. Dkt. Nicas amesema Manispaa itaendelea kusimamia utekelezaji wa maagizo hayo, ikiwemo kuhakikisha maeneo yaliyoathiriwa na majitaka yanasafishwa na mfumo sahihi wa uchujaji na utibaji wa maji taka unajengwa. Katika ziara hiyo, Meya pia alitembelea Kiwanda cha Keds na kukipongeza kwa hatua kilizochukua katika kupanua mtaro kwa urefu wa takribani mita 600. Amekitaka kiwanda hicho kuendelea kushirikiana na jamii na kuongeza urefu wa mtaro huo ili kusaidia kupunguza changamoto ya maji katika eneo hilo. Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Picha ya Ndege wamemshukuru Meya kwa kufika katika eneo hilo na kusikiliza malalamiko yao. Wananchi hao pia wameeleza wasiwasi kuhusu madai ya kuwepo kwa kemikali katika eneo la Kiwanda cha Lake Oil, hasa wakati wa mvua. Akizungumzia suala hilo, msimamizi wa kiwanda hicho ambacho bado kiko katika hatua za ujenzi, amesema kwa sasa hakuna kemikali zinazomwagwa katika eneo hilo, bali mabaki yaliyopo ni ya awali. Dkt. Nicas amemwagiza msimamizi huyo kuhakikisha magari yanatumika kuondoa udongo unaodaiwa kuwa na mabaki ya kemikali na kuweka mchanga mpya, ili kupunguza hatari kwa mazingira na jamii inayozunguka eneo hilo.
Wed, 07 Oct 2026 16:04:04 +0000Influencer marketing shifts from followers to measurable returns
Read the full report from the original source.
RecentlyHow tout turned Sh1,000 daily savings into multimillion assets
Read the full report from the original source.
RecentlyCourt Stops Kalangwa’s Daughter Birungi From Collecting Shs60m Monthly Rent
KAMPALA — The Chief Magistrate’s Court at Mengo has issued an interim injunction stopping Jackline Kobusingye Birungi, a daughter of the late businessman Moses Kaliisa Kalangwa, from collecting or otherwise…
RecentlyNestor Basemera, PhD: The Meat Grinder: Why Classrooms Fail the Character Test
The national examination season is here again. As the Uganda National Examinations Board (UNEB) rolls out its annual sets beginning October 30th with the Primary Leaving Examination (PLE), Ordinary and…
RecentlyFrom sneaking onto his mom’s typewriter at age six to building Europe’s AI supercomputers
Read the full report from the original source.
RecentlyWada chief: Kenya must be 'clean' to be credible
"Kenya calls itself probably 'home of champions', but every home has to have a good host and has to be clean to be credible," Banka told the BBC.
RecentlyKaren Hospital Medical Training College ranked best nursing institution nationally
Read the full report from the original source.
RecentlyMusic executive turns hits into a Sh156 million royalties business
Read the full report from the original source.
RecentlyBurundi : de réfugié au Rwanda à diplômé d’un master à Bruxelles
Read the full report from the original source.
RecentlyKATIBU: BUNGE LA TANZANIA LIPO TAYARI KUSHIRIKIANA NA MABUNGE MENGINE
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Ndugu Baraka Leonard, amesema Bunge la Tanzani lipo tayari kujifunza na kushirikishana uzoefu kutoka mabunge mengine Duniani. Katibu wa Bunge ameeleza hayo Oktoba 7, 2026 wakati akitoa hotuba katika Mkutano wa Makatibu wa Bunge wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU). Makatibu hao wanashiriki Mkutano wa 153 wa IPU unaoendelea jijini Arusha katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC). “Tunatambua kuwa hakuna Bunge linalojua kila kitu, mbinu yetu ni kujifunza kutoka kwa wengine na kushirikishana uzoefu,” amesema. Akizungumia mifumo mbalimbali ya kibunge, amesema hakuna mfumo mmoja ulio bora zaidi ya mwingine na kwamba tofauti ya mifumo hiyo ya kibunge ndiyo inayofanya Umoja huo wa Makatibu wa Bunge kuwa muhimu. “Tunapotazama mifumo tofauti ya kibunge iliyopo hapa, tunakumbushwa kuwa hakuna mfumo mmoja ulio bora zaidi. Wengine mna mfumo wa mabunge mawili, wengine kama Tanzania tuna Bunge moja.Tofauti hii ndiyo inayofanya umoja huu kuwa muhimu sana. “Tunakutana si kupanga ni mfumo gani bora zaidi, bali kuelewa ni nini kinachofanya kazi, kwa nini kinafanya kazi na ni mafunzo gani tunaweza kuyachukua,” amesema katibu wa Bunge. Amesema Umoja wa Makatibu wa Bunge unatoa fursa ya kipekee ya kujifunza kutoka kwa kila Bunge kuhusu taratibu za kibunge, jinsi taasisi za kibunge zinavyohifadhi mwendelezo, kusaidia Wabunge, kukabiliana na mabadiliko na kubaki na ufanisi katika mazingira yanayobadilika kwa kasi. Akizungumzia kuhusu mabadiliko kwenye Mabunge amesema, Bunge la Tanzania linafanyia kazi mazingira ya mabadiliko ya haraka ikiwemo mabadiliko katika ya matarajio ya wananchi, mabadiliko ya kiteknolojia na kuogeza uwazi. “Bunge la Tanzania limeingia katika mfumo wa kidijitali kupitia mfumo wa Bunge Mtandao (e-Parliament), ambao unawawezesha Wabunge kupata nyaraka kwa njia ya mtandao na kufanya kazi bila karatasi. “Pia tumeongeza upatikanaji wa shughuli za Bunge kwa umma. Vikao vya Bunge hurushwa kupitia Televisheni ya Bunge na mitandao ya kijamii. Bunge letu lipo wazi kwa wananchi wanaotaka kufuatilia shughuli moja kwa moja, hasa wanafunzi,” amesema. Katibu wa Bunge aliwakaribisha wageni wote Arusha ambao ni washirika katika usimamizi wa shughuli za kibunge. “Mimi na timu yangu tumeandaa kila kitu kuhakikisha mkutano huu unatoa mazingira muafaka ya kubadilishana uzoefu, kujifunza na kushirikiana kitaalamu. “Arusha kwa muda mrefu imehusishwa na diplomasia, majadiliano, ushirikiano wa kikanda na ushiriki wa kimataifa, Mkutano huu pia unakuja katika wakati muhimu sana katika historia ya taasisi za kibunge nchini Tanzania,” amesema.
Wed, 07 Oct 2026 14:05:37 +0000Tayebwa Urges Businesses to Embrace Tax Compliance, Ethical Practices for Economic Growth
Read the full report from the original source.
RecentlyMuhoozi, South Africa Defence Chief Hold Talks
Read the full report from the original source.
RecentlyFuel Cap Rebound Pushes Dar es Salaam Prices Above Sh4,000
Read the full report from the original source.
RecentlyGermany news: Merz rails against extremism, AfD sympathizers
Read the full report from the original source.
RecentlyGovt steps up multi-agency fight against illicit alcohol, drugs
Latest · Business
RecentlyIlemela Council collects 4.37bn/- in first quarter as it targets 19.25bn/- for 2026/27
MWANZA: ILEMELA Municipal Council in Mwanza region has collected 4.37bn/- out of targeted 19.25bn/- in internal revenue set for the…
RecentlyKisumu man jailed 12 years for killing wife in brutal assault
Latest · NATIONAL NEWS
RecentlyPage 807 of 1141 · 22813 stories