Search the region
22509 stories
DKT. MWINYI: SMT NA SMZ ZINAENDELEA KUTEKELEZA ILANI YA CCM KWA MAENDELEO YA WANANCHI
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zinaendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030 kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kuimarisha uchumi na kuboresha maisha ya wananchi. Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 21 Novemba 2026, katika Kongamano la Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) lililofanyika Gombani, Mkoa wa Kusini Pemba, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwaka mmoja wa muhula wa pili wa uongozi. Amesema Serikali zinaendelea kuimarisha miundombinu, huduma za afya, elimu, maji na nishati, sambamba na kukuza sekta za kilimo, viwanda, utalii na Uchumi wa Buluu ili kuongeza ajira na fursa za kiuchumi kwa wananchi. Aidha, amesisitiza dhamira ya Serikali katika kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri, mifuko ya maendeleo na mafunzo ya ujasiriamali, pamoja na kuongeza ushiriki wao katika nafasi za uongozi na maamuzi. Vilevile, amewataka wanawake wa UWT kuendelea kuwa mabalozi wa maendeleo, kudumisha amani na mshikamano wa kitaifa pamoja na kufikisha changamoto za wananchi katika vyombo husika ili zipatiwe ufumbuzi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Ndugu Mary Chatanda, amesema Jumuiya hiyo inajivunia mafanikio yaliyopatikana katika kuwawezesha wanawake kushiriki katika uongozi na maendeleo ya Taifa kupitia uteuzi wao katika nafasi mbalimbali za maamuzi. Amesema kuongezeka kwa nafasi za uongozi kwa wanawake kumewapa fursa ya kuonesha uwezo wao katika kusimamia majukumu na kuchangia maendeleo ya jamii.
Sat, 21 Nov 2026 14:35:51 +0000VET MARATHON KUPAMBA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UDAKTARI WA MIFUGO SUA
Na Farida Mangube Morogoro Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kinatarajia kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa mafunzo ya udaktari wa mifugo chuoni hapo, kwa kufanya shughuli mbalimbali zitakazohusisha mbio za marathoni, utoaji wa huduma za uchunguzi na matibabu ya wanyama bila malipo, pamoja na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rafael Chibunda, amesema tangu kuanzishwa kwa mafunzo hayo, zaidi ya madaktari wa mifugo 1,580 kutoka ndani na nje ya Tanzania wamehitimu katika chuo hicho. Profesa Chibunda amesema kuwa miongoni mwa shughuli zitakazofanyika katika maadhimisho hayo ni mbio za marathoni, utoaji wa huduma za uchunguzi na matibabu kwa wanyama, uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo linalojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Maendeleo ya Kiuchumi (HEET), pamoja na uzinduzi wa mnara utakaokuwa na majina ya wahitimu wa udaktari wa mifugo wa SUA. Amesema Makamu wa Rais, Mheshimiwa Deogratius Ndejembi, anatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika jengo, kuzindua mnara na baadaye kuhutubia jumuiya ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo pamoja na wakazi wa Morogoro. Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Michezo SUA na msimamizi wa VET MARATHON, Charles Lymo, amesema kuwa mbio hizo zitahusisha umbali wa kilomita tano, 10 na 21, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo na Mifugo, Dkt. Bashiru Ali. Ameeleza kuwa makundi mbalimbali ya wananchi yatashiriki katika mbio hizo na washindi watapata zawadi mbalimbali zikiwemo medali. Aidha, amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo kwa lengo la kuimarisha afya zao. Naye Mkuu wa Ndaki ya Tiba ya Wanyama na Sayansi za Afya wa SUA, Profesa Esron Karimuribo, amesema kuwa katika maadhimisho hayo kutakuwa na huduma za uchunguzi na matibabu ya bure kwa wanyama wa kufugwa pamoja na wanyamapori. Amesema huduma hizo zitatolewa katika halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro, huku akiwahimiza wananchi kujitokeza na kupeleka mifugo yao ili inufaike na huduma hizo. Ameeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya chuo kurudisha shukrani kwa jamii kutokana na ushirikiano unaoendelea kutolewa na wananchi.
Sat, 21 Nov 2026 14:38:26 +0000German President Steinmeier to visit Kenya next week
Steinmeier's programme will include engagements in healthcare, digital services, skills development, arts and culture, nature and biodiversity conservation
RecentlyNta mugore ukwiriye gutinya kujya mu buyobozi kuko igihugu cyamuhaye amahirwe
Read the full report from the original source.
RecentlyF999 app guide for Bangladeshi players
Read the full report from the original source.
RecentlyNyanzaga Mine strikes gold at TMIC 2026 as it readies for its production
DAR ES SALAAM: AFTER 17 years of exploration and construction, the Nyanzaga Gold Project has participated in the Seventh Tanzania…
Recently892 graduates of CUHAS cadre pledge to observe ethics, dignity
MWANZA: 892 graduates of the Catholic University of Health Sciences Bugando (CUHAS) have been instructed to adhere to ethics, dignity…
RecentlyCumi na barindwi bashaka kuyobora akarere kawe baramenyekana uyu munsi
Read the full report from the original source.
RecentlyTanzania lures more investors to establish mineral processing, value addition industries
DAR ES SALAAM: TANZANIA has stepped up efforts to attract more local and foreign investors to establish mineral processing and…
RecentlyEducation Must Go Beyond Personal Success, Kepler College Graduates Told
Read the full report from the original source.
RecentlySALAMU ZA POLE
Sat, 21 Nov 2026 14:02:21 +0000L'IA est-elle un guide spirituel fiable ? Les musulmans sont divisés
Une polémique sur le rôle de l'IA dans l'interprétation des édits religieux fait rage sur les réseaux sociaux, reflétant un débat plus large sur la différence entre l'esprit humain et l'« esprit » d'une machine, la concu
RecentlyCentenary Bank Strengthens Support for Women Entrepreneurs at 2026 Women Enterprise Conference and Innovation Impact Awards
KAMPALA, Uganda – 20th November 2026: Centenary Bank has hosted the Women Enterprise Conference 2026 and Women Innovation Impact Awards, bringing together women entrepreneurs, innovators, business leaders and development
RecentlyKenya braces for intensifying November rains
Experts are warning of the need for communities and government agencies to strengthen preparedness and response mechanisms
RecentlyAliyetarajiwa mwanamke wa kwanza kuongoza UN, aliwa kichwa mara mbili
Soma hapa...
RecentlyRais Samia awatunuku kamisheni maofisa wa JWTZ
Read the full report from the original source.
RecentlyBreaking!! Muhoozi Arrests All Otafiire’s Military Guards, Searches All His Property
Read the full report from the original source.
RecentlyTanzania tables measures to ensure its minerals are value-added before being exported
Read the full report from the original source.
RecentlyRuto fires back at opposition over IEBC criticism
The President defended constitutional institutions against what he termed attempts by politicians to interfere with their operations.
RecentlyGovernment begins construction of sports academy in Busia
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 82 of 1126 · 22509 stories