Search the region
22783 stories
MASAUNI: COP12 ISIISHIE KWENYE AHADI, LETENI MATOKEO
Na Karama Kenyunko Michuzi Tv WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Masauni, ameutaka Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12) kuhakikisha maamuzi yatakayofikiwa yanaelekeza hatua za utekelezaji na kuleta matokeo halisi katika maeneo ya pwani na bahari, badala ya kuishia katika ahadi zisizotekelezeka. Masauni alitoa msisitizo huo leo Oktoba 10, 2026 wakati wa Mkutano wa Watendaji Wakuu na Washirika wa COP12, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Alisema wajumbe wanapaswa kuhakikisha ripoti, tathmini na rasimu za maamuzi zinaonyesha hali halisi ya utekelezaji, mafanikio yaliyopatikana, mapungufu yaliyopo na hatua za pamoja zinazohitajika. “Jukumu lenu si kurekodi shughuli pekee. Ni kubaini nini kimebadilika, wapi utekelezaji unaendelea, wapi kuna mapungufu na ni hatua gani za pamoja zinazohitajika,” alisema. Masauni alisema rasimu za maamuzi zinapaswa kulenga utekelezaji na kila hatua inayopendekezwa iwe na madhumuni yaliyo wazi, mhusika anayehusika, utaratibu wa utekelezaji na msingi wa kufuatilia maendeleo. “Maamuzi ambayo hayawezi kutafsiriwa kuwa hatua za kitaifa na kikanda hayatakidhi uharaka uliopo mbele yetu,” alisema. Alisema nchi wanachama zinapaswa kulenga maamuzi machache, yaliyo wazi na yenye matokeo zaidi badala ya kuongezeka kwa ahadi zenye nia njema lakini zisizotekelezeka. “Tunapaswa kulenga maamuzi machache, yaliyo wazi na yenye matokeo zaidi badala ya kuongezeka kwa ahadi zenye nia njema lakini zisizotekelezeka,” alisema. Masauni alisema mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kupasha joto na kuongeza tindikali katika maji, hali inayotishia miamba ya matumbawe na uvuvi, pamoja na maisha ya jamii za pwani na uchumi wa kitaifa. Alisema uchafuzi wa plastiki unaathiri pwani na bahari, huku matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali yakipunguza akiba ya samaki na kuharibu maeneo ya makazi ya viumbe baharini. “Mahitaji ya rasilimali za bahari yanaongezeka na shinikizo katika mifumo yetu ya ikolojia ya bahari na pwani linaongezeka,” alisema. Alisema Tanzania, katika kipindi cha uongozi wake wa Ofisi ya Mkataba wa Nairobi, imesimamia hatua mbalimbali muhimu, zikiwemo kukamilishwa na kupitishwa kwa Itifaki ya Anuwai ya Bahari na Pwani na Maeneo Yaliyohifadhiwa, Mpango wa Kikanda wa Dharura za Mafuta na Mkakati wa Kikanda wa Plastiki na Kemikali Zinazohusiana. Pia alisema Tanzania imeanza kuandaa Dira na Mfumo wa Utekelezaji wa Kikanda wa BBNJ, huku baadhi ya mifumo hiyo ikitarajiwa kujadiliwa na kupitishwa katika COP12. Masauni alisema changamoto za mazingira zinahitaji majibu yanayounganisha ulinzi na urejeshaji wa mifumo ikolojia na mahitaji ya watu, ikiwamo usalama wa chakula, miundombinu inayostahimili changamoto na shughuli za kiuchumi zinazowajibika. “Mtazamo huu jumuishi ndio msingi wa uchumi endelevu wa buluu na lazima uonekane katika maamuzi yetu,” alisema. Alisisitiza pia ushirikishwaji wa jamii za pwani, wanawake na vijana katika sera na uwekezaji unaoathiri maisha yao, akisema hawapaswi kuwa wanufaika pekee bali pia mawakala wa mabadiliko. “Thamani ya Mkataba huu itapimwa kwa matokeo yaliyopatikana katika maeneo yetu ya pwani na bahari, na si kwa idadi ya mikutano iliyofanyika au maamuzi yaliyopitishwa,” alisisitiza. Masauni alisema maamuzi yatakayofikiwa katika COP12 yataathiri afya ya bahari na ustawi wa watu kwa miongo ijayo, hivyo wajumbe wanapaswa kuwa na mtazamo wa kimkakati, shirikishi na wa kuangalia mbele.
Wed, 07 Oct 2026 06:55:05 +0000Fuel prices rise in October as petrol and diesel become more expensive
Read the full report from the original source.
RecentlyGovt urges citizens to seek legal aid
ZANZIBAR: CITIZENS facing legal challenges have been urged to come forward and use the Legal Aid Week to seek advice…
RecentlyInterview exclusive avec Patrick Sangwa : « Face à l’Algérie, nous avons laissé filer deux points »
Après deux journées dans le Groupe I des éliminatoires de la CAN 2027, les Intamba Mu Rugamba comptent 1 point sur 6. Le sélectionneur Sangwa fait le point.
Wed, 07 Oct 2026 06:54:48 +0000Yemen’s Houthis claim strikes on Aden, Riyadh airports
Read the full report from the original source.
RecentlyIsrael marks third anniversary of October 7 terror attacks
Read the full report from the original source.
RecentlyMwinyi tasks ministers to deliver
ZANZIBAR: ZANZIBAR President Dr Hussein Mwinyi has directed newly appointed ministers and deputy ministers to move beyond their offices, engage…
RecentlyTechnology should make tax compliance easier, VP says
Read the full report from the original source.
RecentlyNew Kenya School of Law admission rules challenged in court
Latest · Business
RecentlyMagari mapya kuboresha huduma wananchi wa kasulu
Read the full report from the original source.
RecentlyMwinyi backs fair labour mobility
ZANZIBAR: ZANZIBAR President Dr Hussein Mwinyi has called on African and Gulf Cooperation Council (GCC+) countries to strengthen cooperation on…
RecentlyIgunga issues 593m/- loans to 55 special groups
TABORA: A total of 55 special groups comprising youths, women and people with disabilities (PwDs) in Igunga District Council, Tabora…
RecentlySt Charles Lwanga marks 40 years, targets self-reliance
St Charles Lwanga Senior Secondary School in Mubende District has been challenged to become self-reliant by its 50th anniversary, as the institution marked 40 years of providing education and vocational skills....
RecentlyWetangula pays tribute to Jeffrey Archer after bestselling author dies at 86
NATIONAL NEWS · 4 hours ago
RecentlyDuale: Kenya will not close borders over Ebola
CS Duale said closing borders could encourage people to use illegal entry points
RecentlyUN, govt renew push for adequate housing
DODOMA: THE United Nations in Tanzania and UN-Habitat have renewed their commitment to ensuring adequate housing for all in Tanzania,…
RecentlyUS death row inmate Christa Pike awake and speaking after failed execution, lawyers say
NATIONAL NEWS · 4 hours ago
RecentlyRC Nyongo aipa tano JWTZ Kisarawe, afurahishwa na uwekezaji uwanja wa mpiga wa miguu
Read the full report from the original source.
RecentlyMASSIVE! Victoria University unveils new campus
KAMPALA — Victoria University plans to build a new campus in Naguru and expects construction to begin this year, the institution's vice-chancellor said on Tuesday. Dr. Lawrence Muganga released architectural impressions.
RecentlyBunha fight back to stun Budiope in Busoga Masaza Cup
Bunha county came from behind to beat Budiope 2-1 at Wembley Ground, while Sanya Edrine’s goal gave Bukooli Namayingo a narrow victory over Bugweri. Bunha…
RecentlyPage 822 of 1140 · 22783 stories