Unganishwa

Search the region

22723 stories

Uncategorized · The Star Kenya

Nigeria mourns as 32 killed in military plane crash

President Bola Tinubu describes the crash as a "painful moment" for the military and the entire nation.

Recently
National · Issa Michuzi

Vodacom Tanzania Yaweka Usalama wa Wateja Mbele Katika Wiki ya Huduma kwa Wateja

Mteja anapokabidhi fedha zake, anaposhirikisha taarifa zake binafsi na hata anapopiga simu kuomba msaada, matarajio yake ni zaidi ya kupata jibu la haraka. Anatarajia pia kuwa salama. Hili ndilo jambo ambalo Vodacom Tanzania imelipa kipaumbele katika Wiki ya Huduma kwa Wateja ya mwaka 2026, inayoanza Oktoba 5 hadi 9, kwa kuwapa wateja nafasi ya kufahamu kwa karibu zaidi hatua zinazochukuliwa kuwalinda wao, fedha zao na taarifa zao binafsi, pamoja na mambo wanayoweza kufanya ili kujilinda. Takwimu zinaonesha kwa nini suala hili ni muhimu. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hadi Juni 2026 kulikuwa na akaunti milioni 87 za huduma za fedha kwa njia ya simu nchini. Katika kipindi hichohicho, TCRA ilirekodi jumla ya majaribio 7,334 ya udanganyifu. Ingawa idadi hiyo ilipungua kwa asilimia 25.29 ikilinganishwa na robo iliyotangulia, bado inaonesha kuwa udanganyifu ni changamoto ambayo watumiaji wa huduma za simu wanahitaji kuwa makini nayo. Kwa Vodacom Tanzania ambayo inatawala soko huduma simu nchini, usalama wa mteja unaanzia kwenye kuhakikisha kuwa mtu sahihi ndiye anayepata huduma kwenye akaunti husika. Usajili wa laini za simu unahusisha uthibitishaji wa alama za vidole dhidi ya taarifa za NIDA, na utaratibu huohuo hutumika wakati wa kubadilisha laini za simu. Mabadiliko ya laini za simu hayawezi kufanyika kwa niaba ya mtu mwingine. “Wateja wetu wanatuamini na kutukabidhi sehemu muhimu za maisha yao ya kila siku, ikiwemo fedha zao na taarifa zao binafsi. Imani hiyo inakuja na wajibu wa kuhakikisha wateja wetu wako salama. Wiki ya Huduma kwa Wateja inatupa nafasi ya kuwaonesha hatua tunazochukua kuwalinda, lakini pia kuwakumbusha kuwa nao wana nafasi kubwa katika kujilinda,” alisema Mkurugenzi wa Kitengo cha Shughuli za Huduma kwa Wateja kutoka Vodacom Tanzania PLC, Harriet Lwakatare. Utaratibu huo unaendelea pia pale mteja anapowasiliana na Huduma kwa Wateja. Kabla ya kusaidiwa, mteja huthibitishwa kuwa ndiye mmiliki wa akaunti. Wakati huohuo, Vodacom inaendelea kuwakumbusha wateja jambo moja muhimu kuhusu usalama wa fedha zao: usiwahi kumpa mtu yeyote namba yako ya siri ya M-PESA, hata kama anajitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa Vodacom. Na pale mteja anapohisi kuwa kuna kitu hakiko sawa, kutoa taarifa mapema kunaweza kusaidia. Timu ya Vodacom Tanzania inayoshughulikia masuala ya udanganyifu hushirikiana na wateja kufuatilia namba za simu au barua pepe zinazohusishwa na tukio lililoripotiwa. Pale inapohitajika, timu hiyo pia hushirikiana na Jeshi la Polisi katika uchunguzi na hatua za kisheria. Kwa sababu hiyo, wateja wanahimizwa kutoa taarifa haraka wanapohisi wamekutana na tukio la udanganyifu, badala ya kusubiri. Hatua za kupata msaada zimerahisishwa. Wateja wanaweza kuwasiliana na Huduma kwa Wateja ya Vodacom kwa kupiga 100 au 101, kutuma ujumbe WhatsApp kupitia +255 754 100 100, kutuma barua pepe customercare@vodacom.co.tz, au kufika katika duka la Vodacom au dawati la Huduma kwa Wateja. Kwa wateja wanaopendelea kujihudumia wenyewe, App ya My Vodacom inawawezesha kupata huduma mbalimbali bila kutumia data. Wateja pia wanaweza kutumia huduma ya kufungua PIN ya M-PESA kila siku. Vodacom Tanzania inawahimiza wateja kufanya usalama kuwa sehemu ya matumizi yao ya kila siku ya simu: kutumia njia rasmi za Vodacom, kuhakikisha wanajua wanayewasiliana naye kabla ya kutoa taarifa au kutuma fedha, na kuripoti mara moja jambo lolote la kutiliwa shaka kupitia Huduma kwa Wateja kwa namba 100. Wateja pia wanaweza kuangalia namba za simu zilizosajiliwa kwa kutumia kitambulisho chao cha NIDA, hatua inayowasaidia kufahamu namba zote zinazohusishwa na utambulisho wao. Wiki ya Huduma kwa Wateja huadhimishwa duniani kote katika wiki ya kwanza kamili ya mwezi Oktoba. Katika maadhimisho ya mwaka huu, Vodacom Tanzania itaendelea kutumia vyombo vya habari na mitandao yake ya kijamii kuwafikishia wateja taarifa muhimu kuhusu usalama, namna ya kupata msaada na hatua wanazoweza kuchukua kujilinda. Kwa sababu huduma nzuri kwa mteja si kuwa tu tayari kusaidia pale tatizo linapotokea. Ni pia kumsaidia mteja kujua namna ya kujilinda kabla tatizo halijatokea. Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania PLC, Harriet Lwakatare (kulia), akizungumza na wateja wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika Duka la Vodacom jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yalilenga kuwathamini wateja na kuhamasisha matumizi salama ya huduma za simu, ikiwemo kutumia njia rasmi za Vodacom na kuripoti vitendo vya kutiliwa shaka kupitia Huduma kwa Wateja kwa namba 100. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania. Tukio hilo lilifanyika Oktoba 5, 2026. Mkurugenzi wa TEHAMA wa Vodacom Tanzania PLC, Athumani Mlinga (kulia), akizungumza na kumkabidhi zawadi mteja wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika Duka la Vodacom jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yalilenga kuwathamini wateja na kuwakumbusha umuhimu wa usalama wanapotumia huduma za simu, ikiwemo kutumia njia rasmi za Vodacom na kuripoti vitendo vya kutiliwa shaka kupitia Huduma kwa Wateja kwa namba 100. Tukio hilo lilifanyika Oktoba 5, 2026. Brigita Shirima (kushoto), Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa Vodacom Tanzania PLC, akimkabidhi zawadi mteja wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika kituo cha huduma cha Vodacom. Maadhimisho hayo yalilenga kuwathamini wateja na kuimarisha uzoefu wao wa huduma. Tukio hilo lilifanyika tarehe 5 Oktoba jijini Dar es Salaam. Harriet Lwakatare (katikati), Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania PLC, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. Maadhimisho hayo yalilenga kuimarisha huduma kwa wateja na kuhamasisha wafanyakazi kuendelea kutoa huduma bora. Tukio hilo lilifanyika tarehe 5 Oktoba jijini Dar es Salaam.

Tue, 06 Oct 2026 02:00:00 +0000
Uncategorized · Daily News

Every market move creates an investment opportunity

DAR ES SALAAM: WHAT if the share price of a company you own falls by 15 per cent tomorrow? Will…

Recently
Uncategorized · Capital FM

NTSA mulls reinstating instant traffic fines from November 26

News · 4 hours ago

Recently
Uncategorized · The Chanzo

Strong Economic Growth, Uneven Gains: Why Tanzania’s Household Incomes Lag?

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

KAMISHNA TANAPA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO SERENGETI

Na Mwandishi Wetu, Serengeti Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Massana Mwishawa, jana, Oktoba 5, 2026, amefanya ziara ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti kwa lengo la kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa katika hifadhi hiyo. Katika ziara hiyo, Kamishna Mwishawa amekagua hatua za utekelezaji wa miradi hiyo ikiwa ni sehemu ya juhudi za TANAPA katika kuimarisha miundombinu ya uhifadhi na utalii pamoja na kuboresha mazingira ya huduma kwa wageni wanaotembelea hifadhi hiyo. Miongoni mwa miradi aliyokagua ni Uwanja wa Gofu wa Hifadhi ya Taifa Serengeti (Serengeti National Park Golf Course), ambao umefikia hatua kubwa ya ukamilishaji na unatarajiwa kuzinduliwa katikati ya mwezi Oktoba mwaka huu. Pia amekagua matengenezo ya Kituo cha Kuongozea Ndege katika Uwanja wa Ndege wa Seronera, pamoja na Kituo cha Kutolea Taarifa kwa Wageni cha Serengeti (Serengeti Visitor Center), kilichojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Ujerumani na kinatarajiwa kuzinduliwa Oktoba 7, 2026. Mradi mwingine uliokaguliwa ni Daraja la Viboko, lililopo katika barabara ya Seronera–Naabi, ambalo ni miongoni mwa miundombinu muhimu inayosaidia usafiri ndani ya hifadhi hiyo. Kwa mujibu wa TANAPA, matengenezo na uboreshaji wa miundombinu ya barabara na madaraja utasaidia kuimarisha shughuli za uhifadhi na utalii, pamoja na kupunguza athari zinazoweza kujitokeza wakati wa msimu wa mvua, hususan kutokana na hali ya hewa ya El Niño. Ziara hiyo pia ilihusisha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Godwell Meng’ataki, ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Magharibi, pamoja na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Ismail Ismail, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Tue, 06 Oct 2026 06:53:59 +0000
Uncategorized · Daily News

When bonds lead: DSE dynamics for investors

DAR ES SALAAM: THE recent trading pattern at the Dar es Salaam Stock Exchange (DSE) raises an important question: Are…

Recently
Uncategorized · Daily News

Speaker Zungu: Why the world must unite to address emerging challenges

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

MBUNGE DKT. MECKTRIDIS MDAKU APEWA TUZO YA HESHIMA KWA KUWAWEZESHA VIJANA WA MALINYI

MALINYI, MOROGORO — Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Dkt. Mecktridis Mdaku, ametunukiwa Tuzo ya Heshima na Mkuu wa Chuo cha Ufundi FDC Sofi, Ndugu Sukaku Jacob, kwa kutambua na kuthamini mchango wake katika juhudi za kuwawezesha vijana wa Malinyi kupata ujuzi na fursa za kujikwamua kiuchumi. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa Mahafali ya 48 ya Chuo cha FDC Sofi yaliyofanyika katika chuo hicho, ambapo jumla ya vijana 150 wamehitimu mafunzo ya ufundi katika fani mbalimbali, kati ya vijana 500 wanaonufaika na mpango wa mafunzo unaolenga kuwawezesha kupata ujuzi wa kitaalamu na kujiajiri. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Chuo hicho, Ndugu Sukaku Jacob, amesema tuzo hiyo ni sehemu ya kutambua mchango wa Dkt. Mdaku katika kuunga mkono juhudi za kuwaandaa vijana kwa kuwapatia elimu ya ufundi na ujuzi unaoweza kuwawezesha kujiajiri na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi. Amesema uwezeshaji wa vijana kupitia elimu ya ufundi ni hatua muhimu katika kukabiliana na changamoto ya ajira na kuongeza fursa za vijana kushiriki katika uzalishaji na maendeleo ya jamii. Mahafali hayo pia yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Dkt. Evaline Munisi, Mkuu wa Wilaya ya Malinyi pamoja na viongozi wengine wa Serikali na wadau wa maendeleo. Katika hotuba zake, viongozi hao wameendelea kusisitiza umuhimu wa vijana kutumia fursa za mafunzo ya ufundi na ujuzi wanazopata ili kujiajiri, kuanzisha shughuli za uzalishaji na kuchangia maendeleo ya familia, jamii na taifa kwa ujumla. Mahafali hayo yamekuja wakati ambapo juhudi mbalimbali zinaendelea katika Jimbo la Malinyi za kuwawezesha vijana kupata elimu, ujuzi na fursa za kiuchumi, ikiwa ni sehemu ya kujenga msingi wa maendeleo endelevu na kuongeza ushiriki wa vijana katika uchumi. Mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo Ndugu Eric Mselo amemshukuru Mbunge Dkt Mecktridis Mdaku kwa moyo wake wa upendo wa kuwawezesha vijana kupata fursa mbalimbali za kujiendeleza kiuchumi na kijamii. Mafunzo haya yatakuwa na faida kubwa kwangu kwani yatanijengea uwezowa kujiajiri mwenyewe. Mafunzo ya ufundi katika Chuo cha FDC - Sofi ni sehemu ya mkakati wa Mhe. Mbunge Dkt. Mecktridis Mdaku katika kuwawezesha vijana wa Malinyi kuweza kunufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi ili waondokane na utegemezi kwenye familia na kuwa na tija katika maisha yao na jamii yao kwa ujumla.

Tue, 06 Oct 2026 06:44:02 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

DG PSSSF: ASANTENI WAAJIRI,TUTAENDELEA KUTOA HUDUMA BORA

Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi (Kulia), Akiwasalimia Wanachama wa Mfuko huo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa wateja Ofisi za Makao Makuu ya PSSSF Dodoma, Oktoba 5, 2026 Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi (Kulia), akimkabidhi cheti cha pongezi Afisa wa PSSSF, Bw. Dolphin Kaizer (katikati), kwa kutambua mchango wake katika kuhakikisha wanachama wanapata huduma bora. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa PSSSF, Bw. Hajji Khamis (kushoto). Cheti hicho amekabidhiwa leo Oktoba 5, 2026 wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Ofisi za Makao Makuu ya PSSSF Dodoma. Picha ya Pamoja ya Watumishi wa Mfuko wa PSSSF Makao Makuu Dodoma, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, Oktoba 5, 2026 Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa PSSSF, Bw. Hajji Khamis (kushoto) akimuhudumia mwanachama wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa wateja Ofisi za Makao Makuu ya PSSSF Dodoma, Oktoba 5, 2026. Afisa wa Huduma kwa Wateja Mwandamizi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Jimmy Kamasho, Kutoka Kanda ya Ziwa Magharibi mkoani Geita, akimuhudumia mwanachama wakati wa Wiki ya Huduma kwa wateja iliyoanza leo oktoba 5, 2026. Dodoma, Oktoba 5, 2026 Katika hali inayoashiria upendo, kuwajali na kutambua mchango wa waajiri mbalimbali, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umejumuika na baadhi ya Waajiri katika uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 na kuwaomba waendelee kuwa mabalozi wazuri wa PSSSF katika maeneo yao ya kazi. Hayo yalisemwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Bw. Paul Kijazi alipokuwa akizindua Wiki ya Huduma kwa Wateja ambayo itaadhimishwa hadi Oktoba 9, 2026. “Kwa namna ya kipekee napenda kutambua uwepo wa Waajiri mbalimbali na kuwashukuru kwa ushirikiano mkubwa mnaotupatia katika maeneo mbalimbali katika kuhakikisha wanachama wa PSSSF wanapata huduma bora na kwa wakati. Na sisi tunaahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kwa maslahi makubwa ya wanachama wetu, asanteni sana kwa kutuunga mkono.” Alisema Bw. Kijazi Bw. Kijazi alisema, kauli mbiu ya mwaka huu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ni Hatua Moja Zaidi ( The Extra Mile), ambapo amewataka watumishi wa PSSSF kufanya yasiyowezekana yawezekane na wajue kwamba kutoa huduma bora kwa wanachama ni wajibu wao wa kwanza, na aliongeza, “Hivyo, tuendelee kusikiliza zaidi wanachama wetu, tuwe wa kwanza kuwafikia wanachama wetu, tutoe elimu sahihi na kwa wakati na tuendelee kutekeleza majukumu yetu kwa uadilifu kama kawaida yetu”. Akizugumzia utoaji huduma kwa wanachama, alisema kuna watumishi wapo katika madawati ya huduma, hao ni pamoja na wenzetu wa kituo cha huduma kwa wanachama, Call Center na Kitengo cha Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, ambao mara nyingi ndio wa kwanza kukutana na wanachama wetu, aliwapongeza na kuwatia moyo waendelee kutoa huduma bora na aliwaomba watumishi wengine wawe tayari kuwasaidia pale wanapohitaji msaada wowote kwa lengo la kumhudumia vyema wanachama wa PSSSF. Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu, Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Hajji Khamis alisema, “Tuwahudumie wanachama wetu kwa usawa, bila kujali nafasi zao, umri wao, eneo wanalotoka au aina ya huduma wanayohitaji. Siku zote tuzingatie muda wa huduma, usahihi wa taarifa,usiri wa taarifa za wateja na kufuata taratibu zetu tulizojiwekea ili tuweze kutoa huduma bora kwa wanachama wetu.

Tue, 06 Oct 2026 06:45:53 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

UBUNIFU WA TANGA UWASA WAWAVUTIA HAZINA,MAMALAKA ZATAKIWA ZIIGE

Na Oscar Assenga,TANGA MSAJILI wa Hazina Nehemiah Mchechu amezitaka mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira nchini kutumia ubunifu wa kutafuta fedha nje ya Serikali, ikiwamo kupitia sekta binafsi na jamii, ili kugharimia miradi ya maendeleo na kupunguza utegemezi wa bajeti ya Serikali. Alitoa wito huo wakati wa ziara ya kutembelea Mradi wa Kuboresha Hali ya Upatikanaji wa Maji Tanga Awamu ya Tatu, unaotekelezwa kwa fedha zilizopatikana kupitia Hatifungani ya Kijani yenye thamani ya Sh53.12 bilioni. Mchechu amesema hatua iliyochukuliwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) inapaswa kuwa mfano kwa mamlaka nyingine za maji nchini katika kutafuta fedha za kutekeleza miradi mikubwa. Alisema wanaiangalia Tanga UWASA kwa wivu mkubwa kutokana na jinsi inavyofanya vizuri hiyo wanataka na taasisi zote za maji kuiga mfano wa Tanga Uwasa Tanga UWASA imekuwa taasisi ya kwanza ya maji nchini Tanzania na katika ukanda wa Afrika Mashariki kufanikiwa kupata na kuorodhesha Hatifungani ya Kijani kwa ajili ya kugharimia miradi ya majisafi, majitaka na uhifadhi wa mazingira. Kwa Mchechu, hatua hiyo inaonyesha kuwa taasisi za umma zinaweza kutumia ubunifu kupata fedha za miradi bila kutegemea Serikali Kuu pekee. Amesema iwapo mamlaka nyingine zitatumia mfumo huo, Serikali inaweza kupata nafasi ya kuelekeza fedha ambazo zingetumika kwenye miradi ya maji katika maeneo mengine ya kipaumbele cha maendeleo. Mchechu, aliyeambatana na Menejimenti ya OTR, amempongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga UWASA, Dk Fungo Fungo, pamoja na menejimenti ya mamlaka hiyo kwa ubunifu huo. Amesema Tanga UWASA ni miongoni mwa taasisi 308 zinazopata usimamizi wa Hazina. Wakati huo huo, utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya Sh53.12 bilioni umefikia asilimia 80. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga UWASA, Mha Salum Ngumbi, amesema mradi huo ulianza Oktoba 12, 2024 na unatarajiwa kukamilika Novemba 30, 2026. Amesema ukikamilika, mradi huo utasaidia kuboresha huduma ya maji kwa wakazi takribani 600,000 wa Jiji la Tanga pamoja na miji ya Muheza na Pangani. Mabayani kuongeza uwezo Ngumbi amesema mradi huo unahusisha upanuzi wa Kituo cha Kusukuma Maji cha Mabayani, ambacho uwezo wake utaongezwa kutoka mita za ujazo 42,000 hadi 72,000 kwa siku. Amesema kazi hiyo itahusisha ufungaji wa mashine nne za kusukuma maji, kila moja ikiwa na uwezo wa kusukuma mita za ujazo 1,500 kwa saa. Pia, bomba kubwa lenye kipenyo cha milimita 600 linawekwa kutoka Mabayani hadi Mowe kwa urefu wa kilomita 6.4. Mowe kuongeza uzalishaji Ngumbi amesema Mtambo wa Kutibu Maji wa Mowe unapanuliwa ili kuongeza uwezo wa kutibu na kuzalisha maji kutoka mita za ujazo 45,000 hadi 60,000 kwa siku. Aidha, mradi huo unahusisha upanuzi wa mtandao wa usambazaji maji kwa kilomita 60 pamoja na ununuzi na ufungaji wa mita 10,000 za maji za malipo kabla. Amesema mita hizo zitasaidia kudhibiti upotevu wa maji na kuimarisha ukusanyaji wa mapato. Majitaka, Mto Zigi vyapewa kipaumbele Katika eneo la majitaka, Ngumbi amesema mradi huo unahusisha uendelezaji wa mtandao kwa urefu wa kilomita 1.5 na ukarabati wa bomba la majitaka lenye urefu wa kilomita tatu katika eneo la Ngamiani. Amesema pia kuna shughuli za uhifadhi wa mazingira zinazolenga kuhakikisha uendelevu wa Mto Zigi. Mradi huo, pamoja na kuongeza uwezo wa uzalishaji na usambazaji wa maji, unalenga kuboresha huduma za majitaka na kupunguza upotevu wa maji, hatua ambayo Tanga UWASA inatarajia kuongeza ufanisi wa huduma na mapato ya mamlaka hiyo.

Tue, 06 Oct 2026 06:47:10 +0000
Uncategorized · Mwananchi

Ujumbe wa Rais Samia IPU, agusia migogoro ya kisiasa

Soma zaidi...

Recently
Uncategorized · Daily News

IPU Secretary General hails Dr Tulia’s leadership

ARUSHA: INTER-Parliamentary Union (IPU) Secretary General Ms Anda Filip has commended IPU President Dr Tulia Ackson for her leadership and…

Recently
Uncategorized · Capital FM

Two injured as tanker explodes at Sachangwan, highway closed

News · 4 hours ago

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Kasneb, Kenya Veterinary Board advertise 15 jobs

Both institutions say they are seeking qualified candidates to fill the advertised positions

Recently
Uncategorized · Capital FM

Court upholds Sh1.7m award against Co-op Bank over vehicle sale

Banks · 4 hours ago

Recently
Uncategorized · Daily News

National Supply Chain Policy charts path to Dira 2050

DAR ES SALAAM: THE ambition to build a competitive, industrialised economy by 2050 places supply chain management at the heart…

Recently
Uncategorized · Daily News

Why companies must stay compliant to protect value

DAR ES SALAAM: FOR a company, complying with registration and reporting requirements is more than a legal obligation. It keeps…

Recently
Uncategorized · UBC

Uganda Hosts First-Ever African Defence Chiefs Conference on Military Operations Other Than War

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Daily News

Geita RC calls for responsible mining, local processing

GEITA: GEITA Regional Commissioner, Mr Alexander Mnyeti has called for responsible investment in the mining sector, urging stakeholders to comply…

Recently

Page 849 of 1137 · 22723 stories