Search the region
22684 stories
MoH, CoG set October 14 deadline for county facility contracts
Latest · Capital Health
RecentlyNBC Yakutana na Wateja Wake Wakubwa Arusha, Yasisitiza Dhamira Yake Ukuzaji Sekta ya Utalii
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya kuchochea ukuaji wa sekta ya utalii nchini kwa kuendelea kuwekeza katika suluhisho za kifedha na kiteknolojia, ubia wa kimkakati pamoja na mipango ya uwajibikaji kwa jamii inayolenga kuunga mkono maendeleo ya sekta hiyo. Dhamira hiyo ilisisitizwa na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NBC, Elvis Ndunguru, wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka kampuni na taasisi mbalimbali jijini Arusha. Hafla hiyo, iliyowakutanisha viongozi na maofisa wa NBC pamoja na wawakilishi wa kampuni na taasisi mbalimbali, ililenga kuimarisha uhusiano kati ya benki na wateja wake, kubadilishana mawazo kuhusu fursa za biashara, kutambulisha huduma na suluhisho mpya za kifedha, pamoja na kupata mrejesho kuhusu namna NBC inavyoweza kuendelea kuboresha huduma zake kulingana na mahitaji ya wateja. Akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa kupitia timu ya Biashara ya benki hiyo (CIB), Ndunguru alisema matukio kama hayo ni sehemu ya mkakati wa benki wa kuwa karibu na wateja wake, kuwaeleza maendeleo katika huduma za kifedha na kidigitali, pamoja na kuunda mazingira yanayowezesha wateja kubadilishana taarifa na fursa za biashara. “Tukiwa kama mhimili muhimu wa utoaji wa huduma za kifedha nchini, NBC tunatambua umuhimu wa kutoa huduma bora na kujenga ushirikiano wa karibu na wateja wetu. Mabadiliko ya kiteknolojia na ubunifu yanaendelea kubadili mahitaji ya wateja, hivyo tunahitaji kuendelea kubuni na kuboresha huduma zetu ili ziendane na mazingira hayo,” alisema Ndunguru. Alitaja baadhi ya maeneo ambayo NBC imeendelea kuboresha kupitia teknolojia kuwa ni mifumo ya ukusanyaji wa mapato na malipo ya serikali, ikiwemo GePG na MUSE, pamoja na suluhisho za ukusanyaji wa malipo kwa taasisi mbalimbali, zikiwemo Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Ndunguru alisema Arusha ni mkoa wa kimkakati kwa NBC, kutokana na nafasi yake katika uchumi wa utalii nchini, huku akieleza kuwa benki hiyo itaendelea kutafuta fursa za kuunga mkono uwekezaji katika utalii pamoja na sekta nyingine muhimu za uchumi kama kilimo na ufugaji. “Arusha ni mkoa wa kimkakati katika utekelezaji wa agenda yetu ya kuhudumia sekta ya utalii. Tutaendelea kuboresha na kuwekeza katika fursa mbalimbali, hususan katika maeneo ya utalii, sambamba na sekta nyingine zenye mchango mkubwa katika uchumi kama kilimo na ufugaji,” alisema. Aidha, Ndunguru alisema NBC inaendelea kutumia matukio kama hayo kujenga mitandao ya kibiashara miongoni mwa wateja wake, huku huduma za kidigitali kama NBC Connect zikitumika kama sehemu ya suluhisho zinazolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa kampuni, mashirika na taasisi za serikali. “Tunaamini kuwa msingi wa huduma za kipekee ni kuelewa mahitaji na matarajio ya wateja wetu. Matukio kama haya yanatupatia mitazamo na mrejesho unaotusaidia kuwa wabunifu zaidi na kuendelea kuboresha uzoefu wa wateja wetu katika huduma za kibenki,” aliongeza Ndunguru. Kwa upande wake, Meneja wa NBC Tawi la Arusha, Mukiza Aggrey Mboneko, alisema NBC inaendelea kutoa huduma mbalimbali zinazolenga kukidhi mahitaji ya wawekezaji na wafanyabiashara katika sekta ya utalii. Alisema huduma hizo zinajumuisha mikopo kwa ajili ya ununuzi wa magari ya kubebea watalii, ujenzi na uendelezaji wa kambi za utalii (camps), lodges na hoteli, pamoja na mitaji ya biashara kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao ndani ya mnyororo wa thamani wa sekta ya utalii. “Pia tuna mifumo ya malipo iliyounganishwa na TANAPA na Ngorongoro, inayowawezesha wadau kufanya malipo mbalimbali, ikiwemo ada za hifadhi (park fees), kwa urahisi zaidi,” alisema Mboneko. Aliwaalika wafanyabiashara na taasisi mbalimbali jijini Arusha kutumia fursa zilizopo kushirikiana na NBC, akisema benki hiyo itaendelea kutoa suluhisho na zana za kifedha zinazolenga kusaidia biashara kukua na kuimarisha ufanisi wa shughuli zao. Baadhi ya wateja wa NBC waliohudhuria hafla hiyo walisema majadiliano hayo yamekuja wakati muhimu, wakati Arusha ikiendelea kushuhudia shughuli kubwa za kiuchumi zinazochochewa na ukuaji wa sekta ya utalii pamoja na biashara, kilimo na viwanda. Miongoni mwao ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Dkt. Ernest Mjingo, ambaye alisema huduma za kisasa za kifedha, hususan mifumo ya kidigitali, zimeendelea kuwa muhimu kwa taasisi na wafanyabiashara katika kurahisisha miamala na ukusanyaji wa mapato. “Kwa sasa Arusha iko katika kasi kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi yanayochagizwa na ukuaji wa utalii, biashara, kilimo na viwanda. Ni jambo zuri kuona NBC, ambayo inahudumia wadau wengi katika sekta hizi, ikiendelea kuwaunga mkono kupitia huduma za kisasa, ikiwemo huduma za kidigitali ambazo zimekuwa msaada mkubwa katika kurahisisha miamala ya kifedha na ukusanyaji wa mapato ya serikali,” alisema Dkt. Mjingo. Mbali na huduma zinazolenga taasisi na biashara, Dkt. Mjingo pia alieleza kuvutiwa na huduma zinazotolewa na NBC kwa wastaafu, akisema huduma hizo zinampa matumaini ya kuendelea kuwa na uhusiano mzuri na taasisi za kifedha hata baada ya kustaafu Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw, Elvis Ndunguru (pichani) akizungumza na wageni waalikwa ambao ni wateja wa benki hiyo jijini Arusha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka makampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Hafla hiyo iliyoandaliwa kupitia timu ya Biashara na Uwekezaji (CIB) ya benki hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha. Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw, Elvis Ndunguru (wa tatu kushoto - waliosimama) akisalimiana na baadhi ya wateja wa benki hiyo jijini Arusha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka makampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Hafla hiyo iliyoandaliwa kupitia timu ya Biashara na Uwekezaji (CIB) ya benki hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha. Baadhi ya wateja wa benki ya NBC jijini Arusha wakifuatilia hafla hiyo Hafla hiyo, iliyowakutanisha viongozi na maofisa wa NBC pamoja na wawakilishi wa kampuni na taasisi mbalimbali, ililenga kuimarisha uhusiano kati ya benki na wateja wake, kubadilishana mawazo kuhusu fursa za biashara, kutambulisha huduma na suluhisho mpya za kifedha, pamoja na kupata mrejesho kuhusu namna NBC inavyoweza kuendelea kuboresha huduma zake kulingana na mahitaji ya wateja. Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw, Elvis Ndunguru sambamba na maofisa wengie wa benki hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa ambao ni wateja wa benki hiyo jijini Arusha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka makampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Hafla hiyo iliyoandaliwa kupitia timu ya Biashara na Uwekezaji (CIB) ya benki hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha.
Mon, 05 Oct 2026 11:30:00 +0000MAADHIMISHO MWEZI WA HUDUMA KWA WATEJA: NBC Yaenda “Extra Mile” Kuwafikia Wateja, Yasisitiza Huduma Zinazoendana na Mahitaji Halisi
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua rasmi Mwezi wa Huduma kwa Wateja 2026 kwa kusisitiza dhamira yake ya kwenda hatua ya ziada katika kuwafikia wateja kwenye maeneo yao ya biashara na shughuli za kiuchumi, kusikiliza mahitaji yao na kutumia mrejesho huo kuboresha huduma na suluhisho za kifedha. Mwaka huu, maadhimisho hayo yanaongozwa na kaulimbiu “Extra Mile – Hatua ya Ziada,” inayolenga kuakisi dhamira ya NBC kwenda zaidi ya utoaji wa huduma za kawaida kwa kuelewa mahitaji ya mteja, kufuatilia changamoto hadi zinapatiwa ufumbuzi na kuendelea kubuni huduma zinazorahisisha maisha na biashara. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NBC, Bi. Alelio Lowassa, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Theobald Sabi, alisema Extra Mile si kaulimbiu ya mwezi mmoja bali ni sehemu ya utamaduni wa huduma ambao NBC inalenga kuutekeleza kila siku. “Kwetu NBC, Extra Mile si kaulimbiu ya mwezi mmoja. Ni namna tunavyotaka kuwahudumia wateja wetu kila siku. Ni kusikiliza na kuelewa hitaji la mteja, kufuatilia jambo hadi lipatiwe ufumbuzi, kuheshimu muda wa mteja, kutimiza ahadi zetu na kuendelea kubuni huduma zinazorahisisha maisha na biashara za wateja wetu,” alisema. Bi. Lowassa alisema NBC imeamua kuendesha maadhimisho hayo kwa mwezi mzima ili kupata muda zaidi wa kusikiliza wateja, kujifunza na kuboresha huduma, huku ikiendelea kuwekeza katika teknolojia na kupanua mtandao wa huduma ili kukidhi matarajio ya wateja wanaohitaji huduma zenye kasi, usalama na urahisi. Alisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita NBC imefungua wastani wa matawi matano mapya kila mwaka, huku mtandao wa NBC Wakala ukifikia zaidi ya mawakala 26,000 nchini. Aidha, benki hiyo imeendelea kuboresha NBC Kiganjani, NBC Connect, GePG na NBC Lipa Namba, pamoja na kurahisisha upatikanaji wa mikopo ikiwemo mikopo ya muda mfupi ya hadi siku 30 kupitia NBC Kiganjani. “Lengo ni moja: kupunguza muda na hatua anazotumia mteja kupata huduma. Hii ndiyo maana ya ahadi yetu ya Daima Karibu Nawe,” alisema. Hafla hiyo pia ilihusisha mjadala maalum wa jopo (panel discussion) uliowakutanisha wateja wa NBC pamoja na wataalamu kutoka maeneo mbalimbali, waliopata fursa ya kujadili uzoefu wao na mchango wa huduma za kifedha katika kukuza shughuli za kiuchumi. Akizungumza kwenye mjadala huo, Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Bw. Benjamin Nkaka, alionyesha kuridhishwa na kasi ya ongezeko la makundi mbalimbali ya kijamii, wakiwemo wakulima, kutumia huduma za bima, ikiwemo bima ya afya na kilimo, hali inayochangiwa na kuongezeka kwa elimu kuhusu umuhimu wa bima na utayari wa jamii kukabiliana na hatari zinazoweza kuathiri shughuli zao za uzalishaji. “Zaidi kwa sasa tunaelekea kwenye mvua za El Niño na Serikali, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, wamewekeza nguvu katika kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari, hususani kwenye maeneo ya miundombinu na mahitaji mengine muhimu ikiwemo chakula. Sisi wadau wa bima tunaunga mkono jitihada hizo kwa kuwahamasisha wananchi wawekeze pia kwenye bima ili waweze kupata ulinzi wa mali zao pindi watakapokumbana na athari za mvua hizo, ili kulinda mitaji, mazao, mifugo na biashara zao,” alisisitiza. Akizungumza kwa niaba ya wateja wengine wa benki hiyo, mfanyabiashara na mteja wa muda mrefu wa NBC, Bw. Assaa Simba Haroun, aliipongeza benki hiyo kwa hatua ya kuwafikia wateja kwenye maeneo yao, akisema wafanyabiashara wanahitaji uangalizi na ushauri wa karibu kutoka taasisi za fedha ili kuwawezesha kuendesha biashara zao kwa ufanisi na kulinda mitaji yao. “Hatua hii ya NBC kuwatembelea wateja wake inakwenda kuondoa changamoto ya muda mrefu inayowakabili wafanyabiashara wengi ambao baada ya kukopeshwa tu taasisi za fedha huwa zinawaacha bila uangalizi wowote hadi pale mambo yanapokwenda kombo. Tunawapongeza sana NBC kwa mkakati huu muhimu unaolenga kuwalea wafanyabiashara wasiwe wapweke dhidi ya changamoto zinazowakabili,” alisema. Akifafanua zaidi kuhusu maadhimisho hayo, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa NBC, Bi. Salama Mussa, aliwashukuru wateja kwa muitikio wao kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo, huku akiwataka wafanyakazi wa NBC kutumia maadhimisho hayo kuwafikia wateja kwenye maeneo yao, kutatua changamoto za kihuduma na kuendelea kuhamasisha matumizi ya huduma za kidijitali ili kuwawezesha kupata huduma kwa kasi, usalama na urahisi zaidi. Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Bi. Alelio Lowassa (kushoto), akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa NBC, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa benki hiyo, wafanyakazi pamoja na wateja wa NBC. Mkurugennzi wa Biashara wa NBC, Bw Jacob Kashimba (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa NBC, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa benki hiyo, wafanyakazi pamoja na wateja wa NBC. Mkurugenzi wa Wateja Wadogo, Elibariki Masuke (alieshika mic) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa NBC, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa benki hiyo, wafanyakazi pamoja na wateja wa NBC. Akizungumza kwenye mjadala huo, Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Bw. Benjamin Nkaka (alieshika mic) alionyesha kuridhishwa na kasi ya ongezeko la makundi mbalimbali ya kijamii, wakiwemo wakulima, kutumia huduma za bima, ikiwemo bima ya afya na kilimo, hali inayochangiwa na kuongezeka kwa elimu kuhusu umuhimu wa bima na utayari wa jamii kukabiliana na hatari zinazoweza kuathiri shughuli zao za uzalishaji. Meneja Mawasiliano na Mahusiano ya Umma Mwandamizi wa benki ya NBC Bi Brendansia Kileo akiongoza mjadala wa wataalam wabobezi (panel discussion) wakati wa hafla wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa NBC, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa benki hiyo, wafanyakazi pamoja na wateja wa NBC. Akizungumza kwa niaba ya wateja wengine wa benki hiyo, mfanyabiashara na mteja wa muda mrefu wa NBC, Bw. Assaa Simba Haroun (pichani) aliipongeza benki hiyo kwa hatua ya kuwafikia wateja kwenye maeneo yao, akisema wafanyabiashara wanahitaji uangalizi na ushauri wa karibu kutoka taasisi za fedha ili kuwawezesha kuendesha biashara zao kwa ufanisi na kulinda mitaji yao. Katika hafla hiyo wateja wa benki ya NBC walipata wasaa kutoa maoni yao kuhusu huduma mbalimbali za benki hiyo. Baadhi ya wateja wakifuatilia hafla hiyo. Hafla hiyo ilihusisha maofisa waandamizi wa benki ya NBC na wateja wa benki ya NBC.
Mon, 05 Oct 2026 15:14:53 +0000Health Ministry Calls for Stronger Accreditation Standards to Improve Patient Safety
Read the full report from the original source.
RecentlyKenya tourism records growth despite faces infrastructure gaps
Read the full report from the original source.
RecentlyGov't, governors strike deal on SHA contracting for county health facilities
Read the full report from the original source.
RecentlyAustralia, New Zealand probe Flydubai pilot's time there
Read the full report from the original source.
RecentlyTANZANIA, AFRIKA NA GCC+ ZAKAZA KUIMARISHA UHAMAJI SALAMA WA NGUVU KAZI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Bi. Zuhura Yunus, kwa niaba ya Katibu Mkuu, Bi. Mary Maganga, akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, ulioanza leo Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam. Wengine pichani kutoka kushoto ni Dkt. Sabelo Mbokazi, Mkuu wa Kitengo Cha Kazi, Ajira, na Uhamaji wa Kamisheni ya Umoja Wa Afrika (AU) Mhe. Sheikha Najwa Bint Abdulrahman Al-Thani, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar na Mhe, Mohammed Hassan Al Obaidli kutoka Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC Bureau) Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Bi. Zuhura Yunus, kwa niaba ya Katibu Mkuu, Bi. Mary Maganga, akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, ulioanza leo Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam. Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Bi. Zuhura Yunus (katikati), kwa niaba ya Katibu Mkuu, Bi. Mary Maganga, akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, ulioanza leo Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam. Wengine pichani kushoto ni Dkt. Sabelo Mbokazi, Mkuu wa Kitengo Cha Kazi, Ajira, na Uhamaji wa Kamisheni ya Umoja Wa Afrika (AU) na Mhe. Sheikha Najwa Bint Abdulrahman Al Thani, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar. Washiriki wa kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira Oktoba 5, 2026 jijini Dar es ssalaam. Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar, Mhe. Sheikha Najwa Bint Abdulrahman Al-Thani, Akizungumza Kwenye kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, ulioanza leo Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam Mhe, Mohammed Hassan Al Obaidli kutoka Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC Bureau), akizungumza kwenye kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, leo Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Fortunatus Magambo (Wapili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda,wakiwa katika ufunguzi wa kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, leo Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam. UJUMBE WA TANZANIA KWENYE ufunguzi wa kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, leo Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam. Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar, Mhe. Sheikha Najwa Bint Abdulrahman Al-Thani (Kulia), akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Bi. Zuhura Yunus, waki wa ufunguzi wa kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, leo Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam. Baadhi Ya Watendaji Wakuu kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano Kwenye kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam. Tanzania yasisitiza utekelezaji wa vitendo katika uhamaji wa nguvu kazi Afrika na GCC+ Asema Tanzania itahakikisha Maslahi ya Wafanyakzi wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi yanalindwa Na OWM (KAM) – Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kulinda haki za wafanyakazi na maslahi ya wahamiaji ili kuhakikisha uhamaji wa nguvu kazi kati ya Afrika na nchi za GCC+ unakuwa salama, wenye haki na wenye tija. Akizungumza leo tarehe 5 Oktoba, 2026 jijini Dar es salaam, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Zuhura Yunus ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo katika Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue uliowakutanisha Makatibu wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika na washiriki kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (Gulf Cooperation Council - GCC) amesema idadi kubwa ya vijana kutoka nchi za Afrika inaendelea kutafuta fursa za ajira katika nchi za nje hususan katika nchi za Ghuba, na kueleza kuwa kuna umuhimu wa kuhakikisha mchakato huo unafanyika kwa usalama na kulinda haki zao. “Mafanikio ya Doha Dialogue hayapaswi kupimwa kwa ahadi na makubaliano pekee, bali kwa hatua zitakazochukuliwa katika kuimarisha mifumo ya uajiri, maslahi, usalama na afya mahali pa kazi, upatikanaji wa haki, kinga ya jamii na mifumo ya takwimu za uhamaji wa nguvu kazi,” amesema Kadhalika, amesema Tanzania ipo tayari kushirikiana na Umoja wa Afrika pamoja na nchi za Ghuba, Jordan, Lebanon na washirika wengine katika kujenga mfumo madhubuti wa ushirikiano utakaosaidia kuimarisha uhamaji salama na wenye staha wa nguvu kazi kati ya Afrika na nchi za Ghuba. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi Qatar, Sheikha Najwa bit Abdulrahman Al-Thani, amesema ushirikiano kati ya nchi za Ghuba na Afrika unapaswa kuimarishwa zaidi sambamda na kubadilishana uzoefu katika kujenga mifumo ya pamoja inayotekelezeka na yenye matokeo. Vilevile, amesema nchi za Ghuba zimepiga hatua katika kuimarisha mafunzo ya ufundi na stadi, hivyo itatumia uzoefu huo kwa kushirikiana na nchi za Afrika katika kuwaandaa vijana wenye ujuzi unaohitajika katika soko la ajira. Naye, Mkuu wa Idara ya Kazi, Ajira na Uhamaji wa Nguvu Kazi katika Tume ya Umoja wa Afrika, Dkt. Sabelo Mbokazi amesema kuongezeka kwa vijana kutoka Afrika, hususan Afrika Mashariki, baadhi ya nchi za Afrika Magharibi na Afrika Kaskazini, wanaokwenda kufanya kazi katika nchi za Ghuba kunaonesha umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya kanda hizo mbili katika kulinda haki na maslahi ya wafanyakazi wahamiaji. Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility) unaratibiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika na washiriki kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (Gulf Cooperation Council - GCC) ukiongozwa na kauli mbiu isemayo “Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na endelevu katika ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+).
Mon, 05 Oct 2026 15:01:51 +0000IPU president sets peace, parliamentary oversight as priorities for successor
Read the full report from the original source.
RecentlyTom Cruise’s Oscar bait drills into oil, geopolitics and climate
Read the full report from the original source.
RecentlySHA tightens licensing rules for contracted hospitals
Read the full report from the original source.
RecentlyAU, regional blocs move to strengthen African Standby Force amid evolving security threats
Latest · Africa
RecentlyRAYVANNY KUTUMBUIZA WABUNGE WA DUNIA MKUTANO WA IPU
Na Seif Mangwangi, Michuzi TV, Arusha Msanii wa muziki wa bongo flava nchini Raymond Mwakyusa maarufu kama ‘Rayvanny’ anatarajiwa kutumbuiza wajumbe wa mkutano wa 153 wa kimataifa wa Mabunge Duniani ulioanza Leo Oktoba5, 2026 Jijini Arusha. Akizungumza mara baada ya kutua katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha uliopo kisongo, Msanii huyo amesema amekuja kuwaonyesha wageni wanaoshiriki mkutano huo utajiri ambao Tanzania inao kupitia muziki. Amesema ni fursa na heshima kubwa ambayo amepewa kuwa mmoja wa watumbuizaji katika mkutano huo pamoja na uwepo wa wasanii wengi nchini lakini yeye ndio kapewa nafasi hiyo. “ Nina furaha sana ya kupata nafasi ya kutumbuiza wageni katika mkutano wa kimataifa wa Mabunge Duniani, niwaahidi tu kuwa burudani nitakayoitoa itaacha historia Tanzania,” ameahidi Rayvanny. Mkutano wa 153 wa umoja wa Mabunge Duniani umeanza Leo Oktoba 5 , 2026 Jijini Arusha ukiwa ni mara ya kwanza tangu kuanzishwa Kwa umoja huo Duniani. Katika mkutano huo ambapo masuala mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo ajenda za watoto, wanawake, vijana na makundi maalum aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson atamaliza muda wake kama Rais wa Jumuiya ya Mabunge Duniani. Spika Dkt Tulia Ackson allichaguliwa kuwa Rais wa 31 wa IPU, Oktoba 27, 2023 katika Mkutano wa 147 wa IPU, uliofanyika katika mji wa Luanda nchini Angola na hivyo kuongoza Jumuiya hiyo Kwa miaka mitatu. Aidha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa kimataifa.
Mon, 05 Oct 2026 14:55:01 +0000ZILIZOBAMBA MITANDAONI | Ahmed Ally na Simba Marathon, Kamwe afurahia maendeleo ya Pacome
Tazama Zilizobamba mitandaoni ikiwa na stori kibao zilizotikisa mitandaoni. Ni Ally Bakari 'Mufti' na timu ya Viwanjani
2026-10-05T14:40:26+00:00INGINGO Z'INGENZI Z'IMPAMVU YO GUSABA GUHINDUZA AMAZINA
Mon, 05 Oct 2026 16:52:38 +0200KCB and ZHSF sign stratergic patnership to enhance access to health care services in zanzibar
ZANZIBAR: KCB Bank Tanzania and the Zanzibar Health Service Fund (ZHSF) have today signed a Strategic Memorandum of Understanding (MoU)…
RecentlyPrimus Ligue : Vision au firmament, les géants à terre – Le classement qui fait trembler les collines
Il a fallu cinq journées. Cinq petites journées pour que le masque tombe et que la vérité, crue et implacable, s'affiche au grand jour. Au terme de cette cinquième levée, le tableau ne ment plus. Il raconte une histoire, une épopée où les hiérarchies chancellent et où un nouvel ordre s'installe
Mon, 05 Oct 2026 14:52:33 +0000INGINGO Z'INGENZI Z'IMPAMVU YO GUSABA GUHINDUZA AMAZINA
Mon, 05 Oct 2026 16:48:37 +0200Les Lions sont tombés à Intwari, et c’est le cœur de ses nombreux supporters qui a saigné
Il y a des défaites qui s'écrivent au tableau d'affichage. Et il y en a d'autres qui s'inscrivent au fer rouge dans la chair de tout un peuple. Ce 04 octobre 2026, au Stade Intwari, ce ne sont pas onze hommes qui se sont effondrés. C'est une dynastie. C'est soixante-neuf ans d'un mythe vêtu de mauve qui, soudain, a vacillé sous une pluie de cinq gifles. 5-0. Le score est brutal. Inconcevable. Presque impudique pour ceux qui portent ce mauve et blanc depuis 1957
Mon, 05 Oct 2026 14:48:54 +0000SHA gives counties 30 days to secure health facility contracts
MOH, CoG and SHA agree on county facility contracts, 90-day payment for clean claims and a 30-day moratorium on five compliance documents as new contracting starts Monday.
Mon, 05 Oct 2026 17:14:37 +0300Page 859 of 1135 · 22684 stories