Unganishwa

Search the region

22611 stories

Uncategorized · Issa Michuzi

TCU YAFUNGUA AWAMU YA TATU YA UDAHILI, PROGRAMU ZENYE NAFASI ZATAFUTWA

Na Janeth Raphael - MichuziTv Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua Awamu ya Tatu na ya mwisho ya udahili wa wanafunzi wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2026/2027, huku waombaji ambao hawakupata nafasi katika awamu zilizopita wakipewa fursa nyingine ya kutuma maombi katika programu ambazo bado zina nafasi. Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Charles Kihampa ametoa TAARIFA hiyo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma Leo ambapo amesema, dirisha la kutuma maombi katika awamu hiyo litakuwa wazi kuanzia leo Oktoba 3 hadi Oktoba 9, 2026, baada ya Tume kupokea maombi kutoka kwa baadhi ya waombaji ambao hawakufanikiwa kupata udahili katika awamu zilizopita pamoja na vyuo ambavyo bado vina nafasi za udahili. Tume imeviagiza vyuo vya elimu ya juu nchini kuendelea kutangaza programu ambazo bado zina nafasi ili kuwawezesha waombaji kufanya uchaguzi na kutuma maombi kwa wakati. TCU imesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kukamilika kwa awamu mbili za awali za udahili, huku ikiwasihi waombaji ambao hawakutuma maombi au hawakupata nafasi katika Awamu ya Pili kutumia fursa hiyo kutuma maombi katika vyuo na programu wanazozipenda. Awamu ya Tatu itafuata ratiba maalum ambapo vyuo vitawasilisha TCU majina ya wanafunzi waliodahiliwa kati ya Oktoba 13 na 14, 2026, kabla ya majina hayo kutangazwa na vyuo husika Oktoba 17, 2026. Aidha, TCU imesema waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Pili, pamoja na wale ambao hawakuthibitisha udahili wao katika Awamu ya Kwanza, wanatakiwa kuthibitisha udahili katika chuo kimojawapo kuanzia Oktoba 3 hadi 19, 2026. Uthibitisho huo utafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi wa simu au kupitia barua pepe ambayo mwombaji alitumia wakati wa kutuma maombi ya udahili. TCU imeeleza kuwa waombaji ambao hawajapokea namba hiyo wanapaswa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe wenye namba maalum ya siri ili kukamilisha mchakato wa kuthibitisha udahili. Pia, waombaji wameelekezwa kufanya uthibitisho kupitia akaunti walizotumia wakati wa kuomba udahili. Orodha ya waombaji waliodahiliwa katika zaidi ya chuo kimoja inapatikana kupitia tovuti ya TCU. Kwa upande mwingine, TCU imekumbusha kuwa masuala yote yanayohusu udahili au uthibitisho wa udahili yanapaswa kuwasilishwa moja kwa moja kwenye vyuo husika. Vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa za waombaji wanaokumbana na changamoto wakati wa kuthibitisha udahili na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa. Kwa ratiba ya Awamu ya Tatu, maombi ya udahili yatafanyika Oktoba 3 hadi 9, vyuo kuwasilisha majina TCU Oktoba 13 hadi 14, kutangaza majina Oktoba 17, huku uthibitisho wa udahili kwa waliodahiliwa zaidi ya chuo kimoja ukifanyika Oktoba 17 hadi 19, 2026.

Sat, 03 Oct 2026 10:15:26 +0000
Health · Issa Michuzi

DKT. MWIGULU AAGIZA UCHUNGUZI MAJENGO YA HOSPITALI YA WILAYA YA BUNDA YALIYOTITIA

▪️︎ Aagiza wahusika kuwajibishwa iwapo uzembe utathibitika ▪️︎ Aelekeza kodi ya klinka iondolewe ili kupunguza bei ya saruji WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameagiza kupatiwa taarifa za uchunguzi kuhusu majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Bunda yaliyotitia, akitaka hatua zichukuliwe dhidi ya waliohusika iwapo itathibitika kuwa kulikuwa na uzembe. Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo leo, Jumamosi, Oktoba 3, 2026, wakati akizungumza na wananchi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Nyamuswa, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Bunda. “Nimeambiwa Waziri wa Afya alishatengeneza timu na ikafanya kazi na TAKUKURU ameshafanyia kazi. Nizipate hizo taarifa ili hawa waliofanya makosa haya wawajibike kule kule walipo. Lazima wawajibike. Hii kuharibu wilaya hii na kuhamishiwa ukaharibu na wilaya nyingine, hii haikubaliki,” amesema. Amesema wakati wa ukaguzi huo amekuta majengo mawili yakiwa yametitia na kupewa maelezo kuwa hali hiyo imesababishwa na uwepo wa maji katika eneo la mradi pamoja na udongo wa mfinyanzi. “Namuuliza kwa nini majengo yametitia? Wanasema kwa sababu yamejengwa karibu na chanzo cha maji. Chanzo cha maji kile kimekuja baada ya kujenga msingi? Si kilikuwepo pale pale? ... Wanasema udongo huu ni wa mfinyanzi,” amesema. Dkt. Mwigulu amesema Serikali itaendelea kufuatilia suala hilo ili kubaini ukweli wa kilichosababisha majengo hayo kutitia na kuhakikisha wananchi hawapati adhabu kutokana na uzembe katika utekelezaji wa miradi ya Serikali. Amesema Serikali pia inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha maeneo yaliyobaki ya ujenzi wa hospitali hiyo ili wananchi waendelee kupata huduma za afya katika eneo lao. Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na kupanda kwa bei ya saruji, ikiwemo kuelekeza kuondolewa kwa kodi kwenye klinka, malighafi inayotumika katika uzalishaji wa saruji. “Nimewaelekeza Mamlaka ya Mapato waondoe kodi kwenye klinka, malighafi inayotumika kwenye uzalishaji wa saruji ili upatikanaji wa saruji uwe wa uhakika na bei iweze kuwa bei himilivu,” amesema. Amesema Serikali inalenga kuhakikisha upatikanaji wa saruji unaendelea kuwa wa uhakika na bei yake inakuwa himilivu kwa wananchi, akibainisha kuwa katika baadhi ya maeneo bei imekuwa ikipanda hadi kufikia zaidi ya Sh. 25,000, Sh. 27,000 na katika baadhi ya mikoa kufikia Sh. 32,000 kwa mfuko. Kuhusu huduma za afya, Dkt. Mwigulu amesisitiza kuwa wananchi hawapaswi kuchangishwa fedha za mafuta kwa ajili ya magari ya Serikali, hususan magari ya wagonjwa yanayotumika kuokoa maisha. “Hatuwezi tukawa na magari ya Serikali yana mafuta, halafu ambulance ya kunusuru maisha ya wagonjwa tuchangishane mafuta. Haya ni mambo ya mazoea ambayo hatutaki kuwa utaratibu wa Serikali,” amesema. Amesema mwananchi yeyote atakayeombwa fedha za mafuta kwa ajili ya gari la wagonjwa anatakiwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili hatua zichukuliwe. Dkt. Mwigulu pia amesisitiza umuhimu wa wagonjwa walio katika hali mbaya kupewa huduma ya dharura mara moja kabla ya kukamilisha taratibu nyingine za kiutawala. “Mgonjwa aliyezidiwa amefika, hatua ya kwanza apelekwe moja kwa moja kwenye kitanda apate huduma. Hata kumwandikisha mtamwandikisha akiwa ameshapata huduma ya kwanza. Kanusuru kwanza maisha yake. Usifanye itifaki kwenye maisha,” amesema. Kuhusu upatikanaji wa dawa, amesema Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba, hivyo amewataka viongozi na watendaji wa afya kuhakikisha dawa zinawafikia wananchi waliokusudiwa na matumizi yake yanafuatiliwa ipasavyo. Hospitali ya Wilaya ya Bunda ilianza kutekelezwa tarehe 8 Mei, 2019, ikiwa ni miongoni mwa hospitali 67 za awamu ya kwanza za halmashauri zilizolenga kusogeza huduma za afya za ngazi ya hospitali karibu na wananchi. Hadi sasa, Serikali imetoa jumla ya Sh. bilioni 5.39 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo. Hospitali hiyo imeanza kutoa huduma mbalimbali, ikiwemo huduma za wagonjwa wa nje, maabara, afya ya uzazi na mtoto, kujifungua, radiolojia, kulaza wagonjwa, huduma za macho, meno na huduma za dharura.

Sat, 03 Oct 2026 10:16:40 +0000
Uncategorized · Capital FM

ODPP: No Criminal Charges Were Preferred Against Four Suspects in rape, robbery case

Latest · ACCESS TO JUSTICE

Recently
Uncategorized · BBC Afrique

Tout ce que vous devez savoir sur la Coupe du Monde Féminine de la FIFA 2027

Nous vous présentons, grâce à notre équipe « Ask Me Anything », tout ce qu'il faut savoir sur la Coupe du monde féminine de 2027.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Germany: Next president should come from east, says official

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Jamhuri Media

Waziri Mavunde akabidhi gari wa mchimbaji maonyesho ya teknolojia ya madini

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Chanzo

Vijana Wabuni Mfumo wa Kidijitali Kudhibiti Taka Dar es Salaam

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Jamhuri Media

Ruhuwiko yaendelea kung’ara mitihani ya kidato cha nne na sita

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Gachagua claims President Ruto’s media outburst stemmed from foiled Mrima Hill Mineral deal

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Exchange Rwanda

Ngozi Okonjo-Iweala:  The African woman at the centre of new global trade order

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Nile Post

Ntungamo warns against low immunisation as uptake measles-rubella campaign targets 90,000 children

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

CCM YARIDHISHWA NA UJENZI WA SKULI YA SEKONDARI KAMA

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Ndugu Abdi Mahamoud Abdi, amesema CCM imeridhishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Skuli ya Sekondari Kama, akieleza kuwa mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa vitendo. Ndugu Abdi ameyasema hayo leo, Oktoba 3, 2026, wakati akiendelea na ziara yake ya kukagua uhai wa Chama hicho pamoja na kusikiliza changamoto za wananchi, ambapo ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Skuli ya Sekondari Kama. Amesema ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya elimu ni miongoni mwa jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza Ilani ya CCM, hatua ambayo inalenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za elimu na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi. Ndugu Abdi ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo sekta ya elimu. Aidha, amesema CCM itaendelea kufuatilia na kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na Serikali, huku akiwataka walimu, wananchi na wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati ili skuli hiyo ianze kutoa huduma kwa wananchi. Kwa upande wake, Mshauri wa Kazi wa mradi huo, Ndugu Abeli Beni, amesema ujenzi wa Skuli ya Sekondari Kama umefikia asilimia 80 na kwamba mradi huo unakadiriwa kugharimu Sh bilioni 3 hadi kukamilika. Amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu. Naye Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Ndg. Laila Burhan Ngozi, amesema mradi huo unaendelea vizuri na kwamba ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wake. Amesema kukamilika kwa skuli hiyo kutasaidia kupunguza changamoto ya msongamano wa wanafunzi madarasani na hivyo kuboresha mazingira ya utoaji na upatikanaji wa elimu katika eneo hilo.

Sat, 03 Oct 2026 09:44:17 +0000
Uncategorized · KBC

Ruto mourns 17 pilgrims killed in Salama road accident

President William Ruto has sent condolences to the families of 17 pilgrims who died in a road accident at Salama along the Nairobi-Mombasa Highway in Makueni County. The victims were…

Recently
Health · Jamhuri Media

Dk Mwigulu akagua mradi wa Hospitali ya Wilaya Bunda

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · TechCabal East Africa

The $100 sandal that sparked a Ghanaian e-Commerce engine

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

MAGHEMBE AZINDUA KITABU CHA MT. FRANSISKO WA ASIZI, AHIMIZA WATANZANIA KUHIFADHI URITHI WA WAFRANSISKANI

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Ngwaru Jumanne Maghembe (Mb.), amezindua kitabu “Saint Francis of Assisi in Tanzania: A Living Presence – Mtakatifu Fransisko wa Asizi: Uwepo Ulio Hai Tanzania”, akieleza kuwa ni nyenzo muhimu ya kuhifadhi historia na mchango wa Wafransiskani katika maendeleo ya Tanzania, hususani katika elimu, afya na huduma za kijamii. Hafla ya uzinduzi ilifanyika tarehe 2 Oktoba 2026 katika ukumbi wa Padre Pio Shrine Pastoral Centre, Msimbazi, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 800 tangu kifo cha Mtakatifu Fransisko wa Asizi. Kitabu hicho kinaelezea historia ya Wafransiskani pamoja na mchango wao katika kuleta maendeleo ya jamii nchini Tanzania. Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Maghembe amesema Tanzania inathamini mchango wa Wafransiskani katika kuleta maendeleo ya jamii na amesisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kushirikiana na taasisi za dini katika utoaji wa huduma na kuimarisha ustawi wa wananchi, huku historia ya Wafransiskani ikiendelea kuwa sehemu muhimu ya urithi wa Tanzania. Uzinduzi huo pia umeangazia nafasi ya urithi wa Wafransiskani katika kujenga madaraja ya urafiki na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Italia, kupitia uhusiano wa watu na taasisi katika nyanja za kijamii, kiutamaduni na maendeleo. Naye Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Giuseppe Coppola, alieleza kuwa kitabu hicho kinaonesha namna urithi wa Mt. Fransisko ulivyojenga daraja la urafiki wa kindugu kati ya Tanzania na Italia, pamoja na kuonesha mchango wa familia ya Wafransiskani katika maendeleo ya kijamii na kiutamaduni nchini. Kwa upande wake, Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe. Nicole Providoli, alieleza historia ya Wafransiskani kutoka Uswisi waliofika Tanganyika mwaka 1921 na mchango wao katika sekta za elimu, afya na maendeleo ya jamii. Alisema mchango huo umekuwa sehemu muhimu ya kuimarisha uhusiano wa kihistoria na ushirikiano kati ya Uswisi na Tanzania.

Sat, 03 Oct 2026 09:26:16 +0000
Uncategorized · The Citizen

Financial literacy gap leaves two in three Tanzanians struggling

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Jamhuri Media

Kadogosa : Uwanja wa Msalato ukamilike kwa muda uliopangwa

Read the full report from the original source.

Recently
National · Jamhuri Media

Serikali yaokoa bilioni 13.77/- katika ugomboaji wa mizigo

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Senate Leaders Call for Skills Audit Ahead of Proposed Lamu Oil Refinery

Latest · Africa

Recently

Page 898 of 1131 · 22611 stories