Unganishwa

Search the region

22597 stories

National · Issa Michuzi

SERIKALI YATOA MAAGIZO MATATU KATIKA MRADI WA KUENDELEZA TASNIA YA MAZIWA

Na Janeth Raphael -MichuziTv Serikali imeweka msisitizo katika usimamizi na utekelezaji wa Mradi wa Kuendeleza Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi, ikitoa maagizo matatu muhimu ikiwemo kukamilishwa kwa wakati kwa tafiti za mradi, ukusanyaji wa taarifa sahihi za utekelezaji pamoja na matumizi sahihi na utunzaji wa vitendea kazi vilivyotolewa. Maagizo hayo yametolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi magari, pikipiki na vifaa vya ugani kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo. Dkt. Bashiru ameyazungumza hayo leo jijini Dodoma, ambapo amesema Ofisi ya Mradi inapaswa kuhakikisha tafiti zinazohitajika zinakamilishwa kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa, sambamba na kuwepo kwa taarifa sahihi, kamili na zinazoaminika kuhusu utekelezaji wa shughuli za mradi. Amesema ukusanyaji wa taarifa kutoka Halmashauri na taasisi zinazoshiriki katika mradi huo unapaswa kukamilika, huku teknolojia mpya zikitumika kuhakiki maeneo ya utekelezaji na walengwa ili kuondoa uwezekano wa taarifa zisizo sahihi au zisizoweza kuthibitishwa. Katika hatua nyingine, Waziri Bashiru amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha vitendea kazi vilivyotolewa vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kutunzwa ipasavyo ili viweze kudumu na kuendelea kuleta tija. Mradi huo umepokea pikipiki 23, ambapo 17 zimetolewa kwa Tanzania Bara na sita kwa Zanzibar, pamoja na magari sita, matatu kwa Tanzania Bara na matatu kwa Zanzibar, sambamba na vifaa mbalimbali vya ugani vitakavyosaidia shughuli za utekelezaji wa mradi. Ameagiza kila chombo kilichotolewa kisajiliwe na kukabidhiwa kwa mtumiaji anayestahili, huku kumbukumbu sahihi za matumizi, matengenezo na ukarabati zikiwekwa. Aidha, amesisitiza kuwa magari hayo yanapaswa kutumika kwa shughuli za mradi pekee, kwa kuzingatia uzito wa mizigo, hali ya barabara na matengenezo ya wakati, wakati pikipiki zikitumika katika ufuatiliaji wa shughuli za mradi kulingana na maeneo yaliyopangwa. Ameonya kuwa atakayekiuka maelekezo hayo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na taratibu. Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Mhe. Suleiman Masoud Makame, amesema mifugo ni sehemu ya maisha na utajiri wa wananchi, hivyo kuna umuhimu wa kuendelea kuchukua hatua za kuimarisha sekta hiyo. Akizungumza katika hafla hiyo, Suleiman Makame amewashukuru viongozi na wadau mbalimbali kwa ushirikiano wao katika utekelezaji wa mradi huo, akisema umevuka hatua ya awali ya dhana na sasa umefikia hatua ya utekelezaji unaohitaji usimamizi madhubuti. Suleiman Makame amesema mafanikio ya mradi huo yanategemea ushirikiano wa viongozi, watendaji na wadau wote, akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa ufanisi na kufikia malengo yaliyokusudiwa. Amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kuhakikisha sekta ya mifugo inaendelea kuimarika, kuongeza tija katika uzalishaji wa maziwa na hatimaye kuleta manufaa yanayotarajiwa kwa wananchi.

Sat, 03 Oct 2026 06:32:55 +0000
Uncategorized · DW Rwanda

Latvia votes in parliamentary election amid rising costs

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Business Daily

Thugge raises compliance fees for non-deposit-taking credit firms

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

10,000 litres of suspected industrial ethanol intercepted in Kiambu

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Raila mausoleum '98% complete', to be handed over next Wednesday

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Karan wins 2026 FIA African Rally Championship in Tanzania

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

17 killed in multiple-vehicle collision at Salama

Several other people sustained injuries in the multiple-vehicle collision

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

G7 to release millions of barrels of oil and diesel after Trump threat

The group of advanced economies said the move would begin immediately and would last for four months

Recently
Uncategorized · The Chanzo

Wadau Wataka Ufumbuzi wa Mkwamo wa Marekebisho ya Sheria ya Ndoa ya 1971

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · PML Daily

dfcu Bank, CFAO Mobility offer full vehicle financing as Toyota launches new RAV4 and Land Cruiser FJ

Customers buying new Toyota vehicles in Uganda can now borrow up to the full value of the vehicle under a financing deal between dfcu Bank and CFAO Mobility Uganda. The two...

Recently
Uncategorized · PML Daily

STUDIOCANAL takes isiZulu drama Shaka iLembe to international buyers

STUDIOCANAL has begun selling Shaka iLembe: Zulu King, an isiZulu-language drama, to buyers outside Africa for the first time. It is the first time the series has been offered to buyers...

Recently
Uncategorized · PML Daily

Ministry clarifies UNITE’s role in teacher education reform

KAMPALA - The Ministry of Education and Sports has clarified the mandate of the Uganda National Institute for Teacher Education (UNITE), saying the institution was established to spearhead reforms in teacher...

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

El Niño rains will arrive from next week – Met

Farmers urged to rely on detailed forecasts issued by meteorological officials

Recently
National · PML Daily

PAC wants government to regulate China Town stores to shield local traders

Members of Parliament on the Public Accounts Committee (Central Government) have asked the government to act on the rapid expansion of China Town retail outlets in Kampala. They argue that the...

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

KICC lights up in tribute to Raila Odinga as nationwide commemorations kick off

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Mwananchi

Jinamizi la EAC wafanyakazi 17,900 wakirudi kortini baada ya miaka 20

Soma hapa...

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Riara University issues statement after viral video of dramatic off-campus assault

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

MP Pukose under fire over threats against those blocking Ugandan-based Kenyans from voting

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · HabariLeo

AFCON yafungua fursa mpya utalii Tanzania

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Mwananchi

Biashara ya pombe saa 24 ‘Kwa Mangi’ yashika kasi Dar

Soma zaidi hapa...

Recently

Page 901 of 1130 · 22597 stories