Unganishwa

Search the region

22579 stories

National · Issa Michuzi

KISHINDO DC MPOGOLO AKIWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM ILALA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala imepokea na kuridhia Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2026, iliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Jonas Mpogolo, huku ikitoa maazimio manane ya kuimarisha utekelezaji wa Ilani hiyo. Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Said Sultan Siddem, amemshukuru Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, akisema imegusa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ilala na kusaidia kupunguza changamoto zinazowakabili wananchi. Akisoma maazimio hayo, Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Jesca Msangi, amesema azimio la kwanza ni kumpongeza Rais Dk. Samia kwa utendaji kazi, uongozi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini. Amesema azimio la pili ni kuwapongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Charangwa Selemani, kwa kuaminiwa na Rais Dk. Samia kuendelea kuwahudumia wananchi wa Ilala. “Azimio la tatu ni kwamba Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala imepokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani, maoni na ushauri wa Kamati ya Siasa ya Wilaya, ambayo ilifanya ziara ya ukaguzi wa miradi na imeridhishwa na kazi kubwa ya utekelezaji iliyofanywa na usimamizi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mpogolo,” amesema Jesca. Amesema azimio la nne ni kuhimiza utunzaji wa miradi yote ya maendeleo iliyotekelezwa, ikiwemo barabara, ili kuzuia uharibifu wake muda mfupi baada ya kuanza kutumika. Amesema Serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi hiyo, hivyo wananchi na viongozi wanapaswa kuwa na elimu ya uzalendo na kutambua umuhimu wa kutunza miundombinu iliyojengwa katika maeneo yao. Kwa mujibu wa Jesca, azimio la tano ni kusisitiza kuwepo kwa mipango madhubuti ya kukabiliana na athari za mvua za El Niño, ikiwemo kukamilisha kwa wakati miradi ya ujenzi wa barabara, madaraja na mitaro, kusafisha mifereji, kuzoa taka na kuwaelimisha wananchi, hasa wanaoishi maeneo hatarishi na mabondeni, kuchukua tahadhari. Azimio la sita ni kuitaka Serikali kukamilisha mchakato wa kufuta hati ya eneo la Kabimita, Mtaa wa Banguro, ili kuwawezesha wananchi kumiliki ardhi yao kihalali. Azimio la saba ni kuwapongeza wabunge na madiwani wote wa CCM kwa utekelezaji wa Ilani ya Chama, huku azimio la nane likisisitiza Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala, kama chombo kikuu cha utekelezaji wa Ilani kwa mujibu wa Katiba ya Chama, kuendelea kutekeleza wajibu wake wa kukagua, kutoa ushauri na maelekezo, kutoa msukumo pamoja na kuutangaza utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali kwa wananchi. DC MPOGOLO Akiwasilisha taarifa hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema mafanikio yaliyopatikana yanatokana na maono ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, pamoja na uwekezaji mkubwa wa Serikali katika miradi ya maendeleo. Amesema moja ya maeneo ya kipaumbele ni maandalizi ya kupokea ongezeko kubwa la wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2028, maarufu kama Double Cohort. ELIMU Mpogolo amesema Wilaya ya Ilala imetenga Sh bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wapatao 85,000 watakaojiunga na kidato cha kwanza. Amesema wilaya hiyo inaendelea na ujenzi wa shule za sekondari zenye majengo ya ghorofa, upatikanaji wa vifaa vya elimu pamoja na kuunda kamati maalumu itakayoratibu na kusimamia maandalizi hayo. EL NIÑO Kuhusu maandalizi ya kukabiliana na mvua za El Niño, Mpogolo amesema hatua mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa, ikiwemo kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara, madaraja na vivuko, kuzibua mitaro na mifereji pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu hatua za kuchukua wakati wa mvua. “Tunataka kuhakikisha barabara zote zinazojengwa pamoja na madaraja vinakamilika kabla ya mvua hiyo kuanza kunyesha, likiwemo Daraja la Segerea–Majumba Sita na Daraja la Bonyokwa, ambayo yako katika hatua za mwisho za kukamilika,” amesema. Amesema hatua za kukabiliana na El Niño zinahusisha maandalizi kabla, wakati na baada ya mvua, huku Jiji la Dar es Salaam likishirikiana na taasisi, wadau na makundi mbalimbali katika kuokoa watu na mali zao. Amesema pia maeneo na vituo maalumu vinaandaliwa kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali, ikiwemo huduma za afya kwa waathirika wa mafuriko. Mpogolo amesema Jiji la Dar es Salaam tayari limetenga fedha kwa ajili ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo, huku akiwataka wananchi wanaoishi maeneo hatarishi, hususan mabondeni, kuhama mapema. USAFI Akizungumzia suala la usafi, Mpogolo amesema Wilaya ya Ilala imeendelea kutekeleza maelekezo ya Rais Dk. Samia pamoja na Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, kwa kulipa uzito mkubwa ajenda ya usafi. Amesema pamoja na kufanya usafi kwa kushirikiana na wananchi na wadau, wilaya imeboresha njia za kuingia na kutoka katika Dampo la Pugu Kinyamwezi na kuwapa wakandarasi wa uzoaji taka muda wa miezi mitatu kuhakikisha wanakuwa na vifaa vya kisasa vya kufanyia usafi. Amesema pia usimamizi wa sheria ndogo za usafi umeimarishwa kupitia kikosi maalumu kinachojumuisha vijana waliopata mafunzo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jeshi la Akiba pamoja na wataalamu wa mazingira. Kikosi hicho kina jukumu la kusimamia utekelezaji wa sheria za usafi, kuwakamata wanaokiuka sheria, kuwatoza faini na kuwafikisha mahakamani pale inapobidi. “Lengo ni kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linakuwa safi na wananchi wanajenga utamaduni wa kuwa wasafi wakati wote,” amesema. UWEZESHAJI WANANCHI Kuhusu uwezeshaji wananchi kiuchumi, Mpogolo amesema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetoa mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 2.4 kwa vikundi vya wajasiriamali, vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Amesema Sh bilioni 22 zipo katika akaunti zikisubiri kukopeshwa kwa walengwa. “Pia Halmashauri imetenga Sh bilioni 6.4 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kuwawezesha wajasiriamali, hususan wanaonufaika na fedha hizi. Katika Kata ya Pugu tunajenga Kituo Atamizi cha Wajasiriamali, ambacho ujenzi wake unagharimu Sh milioni 990.4, kitakachosaidia kutoa mafunzo kwa wajasiriamali hao na kuongeza thamani ya bidhaa zao,” amesema. MAPATO Akizungumzia suala la mapato, Mpogolo amemshukuru Rais Dk. Samia kwa kuwezesha kuimarika kwa ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha miaka minne, ambapo amesema mapato yameongezeka kutoka Sh bilioni 81 hadi kufikia Sh bilioni 171. “Hii ndiyo siri ya ufanisi wa utekelezaji wa Ilani hii. Tunamshukuru Rais Dk. Samia, alipoingia madarakani alitupa utaratibu mzuri wa ukusanyaji wa mapato,” amesema. Amesema Wilaya ya Ilala na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam zimejipanga kuendelea na utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27, huku akiwashukuru viongozi wa CCM Wilaya ya Ilala kwa usimamizi wa utekelezaji wa Ilani ya Chama.

Fri, 02 Oct 2026 13:22:16 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

Behind a Good Night Out Is an Industry Worth Taking Seriously

-1245 reflects on four years of bringing hospitality, music and people together in Dar es Salaam. In Dar, an evening can begin with dinner and end with the whole table singing along to the DJ. Somewhere in between, friends reconnect, someone celebrates a milestone, and plans for “just one drink” become a night worth remembering. For the guest, that experience should feel effortless. Behind it are people working to get the details right: the welcome, the food, the service, the sound and the timing. After four years in business, 1245 Bar, Restaurant & Lounge is reflecting on what it means to create those experiences consistently, and on the wider contribution of hospitality and entertainment to the city. ‘Opening the venue started with a vision. Sustaining it requires listening, adapting and giving people a reason to return. Guests have choices, and every visit is an opportunity to earn the next one. And that is what we strive for each year’ added Opeyemi Sodipe, Chief Operations Manager at 1245. Through its combination of dining, lounge experiences and entertainment programming, 1245 brings several parts of the industry together. Its role extends from hosting guests to creating a setting where music, service and social connection become a shared experience. For 1245, the lesson from four years is that the details matter. A strong lineup can bring people through the door; the experience across the evening shapes what they remember and whether they come back. This thinking is reflected in its upcoming programme, which connects Tanzanian talent with international entertainment while expanding the scale of the guest experience. On Friday, 2 October, a Bongo Flava Night powered by Johnnie Walker will feature Harmonize, Nandy, Abby Chams and Ommy Dimpoz, putting homegrown music at the centre of the programme. Later in the month, 1245 Outside will present 4PLAYS at Superdome Masaki on Saturday, 17 October, featuring Young Jonn and Ms DSF, with a South African dance troupe adding to the performance experience. The event marks the culmination of 1245’s fourth anniversary celebrations. The Alto White Party on Sunday, 18 October, celebrating its sister company, will round off the weekend. The celebrations are supported by Don Julio, Heineken, Air Tanzania and Clouds Media, bringing beverage, transport and media partners into the programme. For guests, the invitation is simple: make time for good company and an evening out. Table enquiries for 4PLAYS can be made through 1245’s official booking channels, with early-bird tickets available at 4plays.1245tz.com 0r +255 748 211 245 This is chess not checkers.

Fri, 02 Oct 2026 13:11:52 +0000
Uncategorized · The Citizen

Railways corporation, workers' compensation fund ink Sh65 billion four-star hotel, conference project

Read the full report from the original source.

Recently
Health · The Nile Post

Govt Commits to Addressing Hospital Staffing Gaps as Radiographers Cry Out

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Man, 72, drowns after falling into well in Homa Bay

Police said the man slipped and fell into the well while crossing through a homestead.

Recently
Uncategorized · HabariLeo

VETA, BGC kushirikiana kukuza ujuzi

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Citizen

Households face renewed strain as cost of living rises

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Kindiki to illicit alcohol sellers: Your days are numbered

He said says the government had intensified efforts to eliminate illicit and harmful alcoholic drinks from the market

Recently
Sports · Citizen Digital

Man City confirm appeal after Premier League charges verdict

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · KBC

Wamatangi loses bid to stop Ksh813 million EACC recovery case

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

East African Businesses Seek Bigger Share of China Trade

Latest · Banks

Recently
Uncategorized · Azam TV Videos

MAHOJIANO MAALUM | Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti na Utawala wa Michezo (CSRG), Godfrey Ngumbi

Azam TV

2026-10-02T12:43:35+00:00
Uncategorized · Capital FM

Greatness in the works: Omondi outlines desire to transform Kenya Pipeline into African giants

Latest · Sports

Recently
National · HabariLeo

Serikali yazindua mwongozo elimu ya fedha kwenye mitaala

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Business Daily

Health agencies cut pending bills by Sh31bn in a year

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Observer Uganda

Backlog: 132 cases resolved in one week under plea bargain

At least 132 cases have been resolved within a week through Alternative Dispute Resolution (ADR) as the Judiciary moves to reduce case backlog and decongest…

Recently
Uncategorized · Business Daily

Airtel Money bets on low fees against M-Pesa as market matures

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Sifuna hits back at Ruto over Dangote agreement

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

The Last Hurrah: Inside The Rehearsals As Capital FM Gears Up For Tomorrow’s ‘Third Flow Experience @30’

Entertainment · 5 hours ago

Recently
Uncategorized · HabariLeo

Kituo kipya kuongeza huduma za meno

Read the full report from the original source.

Recently

Page 910 of 1129 · 22579 stories