Search the region
22511 stories
VIJANA 90 WABEBA MATUMAINI YA TAIFA KATIKA SAFARI YA ELIMU ALGERIA
Haijawahi kutokea wanafunzi 90 kupelekwa kusoma nje ya nchi na Serikali kwa wakati mmoja. Kupitia Programu ya Samia Scholarship Extended, vijana hao wanakwenda Algeria kupata maarifa na ujuzi katika fani za sayansi na teknolojia, hatua inayochangia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, Toleo la 2023, na Dira 2050 kwa kujenga rasilimali watu yenye umahiri wa kuchochea maendeleo endelevu. Akizungumza Novemba 20, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa kuwaaga wanafunzi hao, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesisitiza kuwa wamechaguliwa kwa ufaulu wao katika masomo ya sayansi kidato cha sita, bila upendeleo. “Mmechaguliwa kwa sababu mmekuwa nyota katika mitihani yenu,” amesema, akifafanua kuwa ufadhili huo si mkopo, bali ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuwaendeleza vijana wenye uwezo mkubwa. Prof. Mkenda amesema uwekezaji katika sayansi na teknolojia unalenga kuijengea Tanzania uwezo wa kuendeleza sekta zake kwa kutumia wataalamu wake. Akitolea mfano reli, ameeleza kuwa kuwa na reli ni maendeleo, lakini kuweza kuijenga wenyewe ndiyo msingi wa maendeleo endelevu, huku akiwahimiza wanafunzi wengine kusoma kwa bidii ili kunufaika na fursa zinazotolewa na Serikali. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, amesema wanafunzi hao wamebeba matumaini ya Taifa katika kuimarisha uwezo wa nchi kwenye sayansi na teknolojia. Amewataka kuitumia fursa hiyo kujijengea maarifa na ujuzi watakaoutumia kutatua changamoto za jamii na kuchangia maendeleo ya Tanzania baada ya kuhitimu masomo yao. “Mmetumwa na Taifa. Taifa zima limewatuma,” amesisitiza Mhe. Wanu, akiwataka vijana hao kusoma kwa bidii, kutii sheria za Algeria, kudumisha maadili na uzalendo, pamoja na kusaidiana licha ya kwenda katika vyuo tofauti. Aidha, amewaomba wazazi kuendelea kuwashauri na kuwaombea watoto wao ili wakamilishe masomo na kurejea salama kulitumikia Taifa. Naye Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare Matinyi, amesema manufaa ya ushirikiano wa elimu kati ya nchi hizo yanaonekana kupitia wahitimu wanaohudumu kama madaktari bingwa, wahadhiri, wahandisi na wataalamu wa TEHAMA nchini na katika kampuni za kimataifa. Amesema mafanikio hayo yanaonesha ubora wa elimu inayotolewa Algeria na umuhimu wa kuendelea kutumia fursa hizo kuandaa wataalamu wanaohitajika kwa maendeleo ya Tanzania. Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Ushauri ya Programu ya Samia Scholarship, Prof. Raphael Chibunda, amesema kamati inashirikiana na Wizara pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutafuta nafasi katika vyuo bora duniani. Amewahimiza Watanzania waishio nje ya nchi, hasa wanaofanya kazi katika vyuo na taasisi za kimataifa, kutumia uzoefu na mahusiano yao kusaidia kuongeza fursa za masomo kwa vijana wa Kitanzania. Akitoa ushuhuda wake, mnufaika wa programu hiyo, Hosea Gideon Ngalama, aliyesoma Shule ya Sekondari Kimamba iliyopo Kilosa, mkoani Morogoro, amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kumwezesha kuendelea na elimu kupitia ufadhili huo. Amejivunia kutoka katika shule ya Serikali na kupata nafasi hiyo, akieleza kuwa inaonesha namna Serikali inavyowajali vijana na kuwawezesha kutimiza ndoto zao za elimu.
Fri, 20 Nov 2026 17:09:44 +0000Bujumbura : le choléra progresse, les habitants demandent une action urgente
Read the full report from the original source.
RecentlyIEBC hits out at opposition after talks walkout
“Walking away from dialogue before substantive discussions begin does not advance the resolution of electoral concerns,” Ethekon said
RecentlyKigali Fight Night ku nshuro ya gatatu igiye kubera mu Rwanda
Read the full report from the original source.
RecentlyIEBC hits out at opposition over walkout from poll talks
“Walking away from dialogue before substantive discussions begin does not advance the resolution of electoral concerns,” Ethekon said
RecentlyLeading causes of court adjournments
The absence of witnesses is the leading cause of court adjournments in Kenya, accounting for 10.5 per cent of all adjournments
RecentlyHalmashauri kuimarisha utekelezaji wa sera na mwongozo wa kurejesha wanafunzi walioacha shule
Read the full report from the original source.
RecentlyDP Kindiki urges broad-based leaders to close ranks, avoid political divisions
Read the full report from the original source.
RecentlyNewly appointed TSC CEO Cheptumo Ayabei assumes office
Read the full report from the original source.
RecentlyBalozi Qatar awanunulia tiketi mashabiki kuisapoti Serengeti Boys Kombe la Dunia U17
KUTOKA QATAR: “…tutawapiga Coasta Rica 3-0, hatutakuwa na huruma” Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Habibu Awesi Mohamed, amenunua tiketi 100 pamoja na jezi kwa ajili ya watanzania wanaoishi nchini humo, ili kwenda kuiunga mkono timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys. Hatua hiyo inalenga kuwapa nafasi watanzania hao kujitokeza kwa wingi uwanjani kesho, kushangilia na kuipa hamasa timu hiyo itakapokabiliana na Costa Rica katika mchezo wa michuano ya Kombe la Dunia U17 inayoendelea nchini humo. Balozi amesema nchini humo tayari kuna mashabiki watanzania takriban 250 na ameelza jinsi walivyojipanga kufika dimbani… Mchezo huo utapigwa kesho Novemba 21 saa 10:00 jioni na utakufikia mbashara kupitia #AzamSports5HD #FIFAU17WorldCup2026 #U17WC #FIFAU17WC #Qatar2026 #SerengetiBoys
2026-11-20T16:31:19+00:00Koome reveals how Supreme Court land was grabbed as Judiciary gets title
Read the full report from the original source.
RecentlyBroad-based leaders defend IEBC as ODM presses for Deputy President position
Read the full report from the original source.
RecentlyShivo Tanzania’s Richard Ashby elected to ZATI board of directors
Read the full report from the original source.
RecentlyNigeria moves to end jail terms for attempted suicide
The Senate bill also seeks to replace criminal penalties for attempted suicide with medical treatment, rehabilitation and support.
RecentlySERIKALI YATENGA SHILINGI BILIONI 200 KUCHOCHEA UJASIRIAMALI KWA VIJANA NA WANAWAKE.
Serikali imetenga Shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kuwawezesha vijana na wanawake kiuchumi kupitia mitaji ya kuanzisha na kuendeleza miradi ya uzalishaji na huduma, hatua inayolenga kukuza ujasiriamali, kuongeza ajira na kupanua ushiriki wao katika uchumi wa Taifa. Akizungumza Novemba 20, 2026, katika Mahafali ya 40 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Kampasi Kuu Dodoma, Naibu Waziri wa Fedha, Laurent Luswetula (Mb.), aliyemwakilisha Waziri wa Fedha, amesema Serikali imeimarisha uwezeshaji huo kupitia Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana kwa kuanzisha Programu ya Kitaifa ya Uwezeshaji Vijana Kiuchumi. Amesema programu hiyo inalenga kuwapatia vijana mitaji ya kuanzisha na kuendeleza miradi katika sekta mbalimbali, huku akiwataka wahitimu kutumia elimu na ujuzi walioupata kubuni biashara zenye tija zinazotatua changamoto za jamii na kukidhi mahitaji ya soko. Aidha, amewataka vijana kuunda au kujiunga na vikundi vinavyokidhi vigezo, kujisajili katika mifumo ya manunuzi ya umma ikiwemo Mfumo wa Kielektroniki wa Manunuzi ya Umma (NeST), pamoja na kujifunza namna ya kuandaa na kuwasilisha zabuni ili kunufaika na fursa za Serikali. Luswetula amesema Serikali imezielekeza taasisi zote za umma kuhakikisha makundi maalum, yakiwemo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, yanapata angalau asilimia 30 ya thamani ya manunuzi yote ya bidhaa, huduma na kazi zinazohitajika kwa mwaka. Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, amesema chuo kitaendelea kuimarisha ushirikiano na taasisi za umma na binafsi pamoja na mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutekeleza miradi ya kimkakati na kutoa huduma za ushauri elekezi kwa ufanisi na weledi. Amesema miongoni mwa miradi inayotekelezwa na chuo hicho kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania ni mradi wa kuimarisha ufuatiliaji na usalama wa shughuli za baharini katika maji ya pwani ya Tanzania, unaozingatia athari za mgogoro wa Bahari ya Shamu. Ameeleza kuwa kupitia mradi huo, chuo kimevijengea uwezo zaidi ya vikundi 20 vya wananchi, hususan wanawake na vijana, katika Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, kuhusu shughuli za kilimo cha mwani. Naye Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la chuo hicho, Prof. Joseph Kuzilwa, amewataka wahitimu kutumia maarifa na ujuzi walioupata kutatua changamoto za jamii, kuchochea ubunifu na kuleta mabadiliko chanya katika maendeleo ya Taifa. Amesema wahitimu wanapaswa kuwa wataalamu wenye weledi, uadilifu, uwajibikaji na uzalendo, huku wakitumia changamoto kama fursa za kujifunza, kubuni suluhisho na kujiletea maendeleo kupitia ajira au kujiajiri. Katika mahafali hayo, chuo kimewatunuku jumla ya wahitimu 6,076, wakiwemo wanaume 2,741 na wanawake 3,335.
Fri, 20 Nov 2026 16:40:37 +0000Kingdom Night: Abagore babiri bagiye gushaka intama zazimiye
Read the full report from the original source.
RecentlyMugabo wanjye jya kurwanirira igihugu - Dore icuruzwa ry'abasirikare mu Burusiya
Read the full report from the original source.
RecentlyNous ne pouvions pas nous offrir une maison pour notre famille, alors nous en avons acheté une avec des inconnus
Au Canada, des personnes et des familles ne peuvent pas se permettre d'acquérir un logement en raison de ses prix élevés et cherchent à s'associer à d'autres personnes se trouvant dans la même situation.
RecentlyURA Relocates Gulu Office to Green Valley, Layibi City Division
Read the full report from the original source.
RecentlyGachagua rejects Bomas as final tallying centre for 2027 presidential results
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 94 of 1126 · 22511 stories