Unganishwa

Search the region

22511 stories

Uncategorized · The Standard

Outrage as KDF officers detain human rights team along Malindi-Lamu highway

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · SoftPower News

dfcu Bank Hails Debut Serena Captain’s Putter Golf Tournament

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

'This is normal for us in Africa,' Dangote dismisses court order halting Lamu oil refinery construction

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Dangote refinery shares to be open to all Kenyans, Ruto assures

Latest · Business

Recently
Business · Issa Michuzi

STANBIC BANK YASEMA MABORESHO YA SOKO LA MITAJI TANZANIA YANAFUNGUA FURSA MPYA KWA TAASISI ZA UMMA

Benki ya Stanbic Tanzania imesema maboresho ya hivi karibuni katika soko la mitaji nchini yamefungua fursa mpya na muhimu kwa taasisi za umma kupata fedha za muda mrefu kwa ajili ya miradi ya kimkakati. Benki imetoa kauli hiyo wakati wa Mkutano wa Nne wa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum) 2026 ulioanza Jumatatu jijini Arusha. Zaidi ya wenyeviti wa bodi na wakurugenzi wakuu 700 wa taasisi za umma wanakutana katika mkutano huo wenye kaulimbiu “Mashirika ya Umma Yenye Ufanisi wa Juu kwa Uchumi Shindani, Shirikishi na Imara katika Kutekeleza Dira 2050.” Chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Tanzania imechukua hatua muhimu mwaka huu katika kuimarisha masoko yake ya fedha. Mwezi Agosti mwaka huu, Benki Kuu ya Tanzania ilitangaza kuwa hati fungani za muda mfupi na hati fungani za Serikali, ambazo tayari zilikuwa wazi kwa wawekezaji wa Kitanzania, sasa zimefunguliwa pia kwa wawekezaji wa kigeni. Aidha, Serikali imetangaza mipango ya taasisi za umma kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), hatua ambayo itawapa Watanzania fursa ya kumiliki hisa katika taasisi zinazowahudumia. “Dira 2050 imeweka azma iliyo wazi kwa Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kipato cha kati cha juu na kuwa na uchumi wa dola trilioni moja ifikapo mwaka 2050. Taasisi za umma zina nafasi muhimu katika safari hiyo.” alisema Elias Ngunangwa, Mkuu wa Mahusiano na Wateja Wakubwa, Stanbic Bank. “Maboresho ya Serikali yanajenga mazingira imara zaidi kwa uwekezaji na mitaji ya muda mrefu. Kama taasisi za kifedha, jukumu letu ni kuleta utaalamu wetu, mitandao yetu na uwezo wetu wa kifedha sambamba na azma hiyo ya Taifa. Tupo tayari kushirikiana na Serikali katika kuitekeleza,” aliongeza. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Stanbic imetoa zaidi ya dola za Marekani bilioni 1 katika ufadhili wa maendeleo nchini Tanzania, ikisaidia miradi ya miundombinu, nishati na biashara. Euromoney imeitaja Stanbic kuwa Benki Bora ya Uwekezaji Tanzania kwa miaka sita mfululizo, huku Soko la Hisa la Dar es Salaam hapo awali likiitambua kama benki bora ya huduma za uhifadhi wa dhamana. Ikiwa sehemu ya Standard Bank Group, Stanbic inaunganisha taasisi za Tanzania na mitaji pamoja na utaalamu kutoka Afrika na maeneo mengine duniani. Stanbic imesema itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Benki Kuu ya Tanzania, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, Soko la Hisa la Dar es Salaam, pamoja na taasisi za umma, kusaidia hatua inayofuata ya maendeleo ya soko la mitaji. Benki hiyo ni miongoni mwa wadhamini wa Mkutano wa Mwaka huu, ambao utaendelea hadi Jumatano, 30 Septemba 2026. Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (alieketi) akisalimiana na Mkuu wa Mahusiano ya Wateja Wakubwa, Benki ya Stanbic, Elias Ngunangwa, wakati wa Mkutano wa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma (C-CEOs Forum) 2026 unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), jijini Arusha. Anaeshuhudia ni Meneja Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano wa benki hiyo, Dickson Senzi.

Tue, 29 Sep 2026 08:30:00 +0000
Uncategorized · SoftPower News

Museveni Calls for Preservation of African Culture & Indigenous Knowledge

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

DCEA YATOA ONYO KWA MAGARI YA MSIBA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA

-Kamishna Jenerali Lyimo atoa angalizo kwa familia, wamiliki wa mabasi Na Mwandishi Wetu FAMILIA zinazokodi mabasi madogo (hiace/coaster) kusafirisha waombolezaji au miili ya marehemu kwenda mikoani zimetakiwa kuwa waangalifu, baada ya kubainika baadhi ya gari hizo zinatumika kusafirisha Dawa za kulevya. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) ni kwamba kuna magari yanayotumika kubeba miili ya marehemu yamekuwq yanabeba Dawa za kulevya wakati wa kwenda au kurudi. Akizungumza leo Septemba 29,2026 jijini Dar es Salaam amesema Mamlaka imebainika kuna magari yanayotumika kusafirisha miili ya marehemu na wanafamilia yanatumika kusafirisha dawa za kulevya, hivyo mamlaka itachukua hatua kali kwa mujibu wa sheria. “Iwapo tutabaini gari inayosafirisha maiti imebeba dawa za kulevya hatutasita kuchukua hatua, tutakama gari,familia na kuzuia maiti.Wanaotumia magari hayo wengine wanasafirisha dawa wakati wanaenda mkoani au wanarudi. Magari hayo mengi ni yale yanayokwenda kanda ya Kaskazini Tanga, Kilimanjaro na Arusha.” Pia amesema kuongezeka kwa matumizi ya magari ya abiria katika usafirishaji wa dawa za kulevya ni jambo linalotia wasiwasi mkubwa, huku wasafirishaji wakitumia huduma za kawaida za usafiri kusafirisha dawa hizo kati ya mkoa na mkoa. Amewataka wamiliki na waendeshaji wa mabasi madogo, mabasi makubwa na magari binafsi kuimarisha udhibiti wa mizigo inayobeba katika magari yao, akionya kuwa gari lolote litakalobainika kutumika kusafirisha dawa za kulevya litatafishwa. "Hatua hii inaweza kuwaacha wamiliki wa magari wasio na hatia wakipata hasara za kifedha, hasa pale ambapo wameshindwa kusimamia ipasavyo jinsi magari yao yanavyotumiwa," amesema Kamishina Jenerali Lyimo. Ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuwa waangalifu wanapokodi magari, hasa kwa ajili ya shughuli za msiba na shughuli nyingine za kijamii, na kuweka makubaliano ya wazi na waendeshaji kuhusu mizigo na vifurushi vingine. Wakati huo huo DCEA imeendelea kufanya operesheni maalum katika mikoa 14 kati ya Julai na Septemba MWAKA huu na kufanikiwa kukamata dawa za kulevya kilo 18,078.41. Mikoa iliyohusika katika operesheni hizo ni Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara, Dodoma, Mbeya, Lindi, Mtwara na Ruvuma. Kati ya dawa zilizokamatwa, kilo 11,504.76 zilikuwa ni bangi, kilo 6,529.5 mirungi, kilo 44.45 bangi aina ya skanka na gramu 41.25 za heroin huku jumla ya watuhumiwa 289 walikamatwa, ambapo 169 kati yao wamefikishwa mahakamani.Wengine taratibu za kisheria dhidi ya wengine zikiendelea. Operesheni hizo pia zilifanikisha ukamataji wa magari mepesi manane, bajaji moja na pikipiki 40 zilizohusishwa na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Tue, 29 Sep 2026 15:41:50 +0000
Uncategorized · Mwananchi

DC Msando aagiza madereva kuondoa mabasi Stendi ya Magufuli

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo (DC), Albert Msando amewaagiza abiria waliopo katika Stendi ya Mabasi ya Magufuli, Dar es Salaam kuingia kwenye mabasi waliyokatia tiketi ili kupata maelekezo kuhusu...

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Iraq: US withdrawal leaves security questions

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Met forecasts rain across 32 counties this week

Meteorologists continue to assess how ocean conditions will influence rainfall during the October-December period.

Recently
Uncategorized · Watchdog Uganda

Beyond the Failures: Kumumanya urges journalists to tell Uganda’s local government development story

Why roads, markets, health centres and schools deserve the same scrutiny as local government failures KAMPALA — Uganda’s development journey has evolved over decades, with the decentralisation system introduced in…

Recently
Uncategorized · Watchdog Uganda

New era for Tooro as President Museveni presides over coronation of Omukama Nyabongo I

President Yoweri Kaguta Museveni today presided over the coronation of His Royal Highness Edward Rukidi Nyabongo I as the 15th Omukama of Tooro, ushering in a new chapter for the…

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

UDA postpones Mombasa ward polls to October 8

UDA said the change was due to the ongoing presidential development tour and official engagements in the county

Recently
Business · Business Daily Africa

Saccos cut bad loans by Sh10bn in a year

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

OPERESHENI MAALUM YANASA DAWA ZA KULEVYA KILO 18,078.41

Na Said Mwishehe,Michuzi TV MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata jumla ya kilogramu 18,078.41 za dawa za kulevya, katika operesheni zilizofanyika katika mikoa 14 nchini katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2026. Operesheni hizo zilifanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara, Dodoma, Mbeya, Lindi, Mtwara na Ruvuma. Akizungumza leo Septemba 29,2026 jijini Dar es Salaam Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema Kati ya kiasi hicho kilichokamatwa kilo 11,504.76 zilikuwa bangi, kilogramu 6,529.5 mirungi, kilogramu 44.45 bangi aina ya skanka na gramu 41.25 heroin. Pia Katika operesheni hizo, jumla ya watuhumiwa 289 walikamatwa, ambapo 169 wamefikishwa mahakamani, huku taratibu za kisheria zikiendelea dhidi ya watuhumiwa wengine. Ameongeza operesheni hizo zimewezesha kukamatwa kwa magari nane, bajaji moja na pikipiki 40, ambazo zilitumika katika shughuli zinazohusiana na usafirishaji wa dawa za kulevya. “Kufuatia operesheni hizo, bangi imeendelea kuongoza kwa kiwango cha uzalishaji na ukamataji, hususan katika mikoa ya Morogoro na Tabora. Mkoani Morogoro, jumla ya kilogramu 6,299.24 za bangi pamoja na kilogramu 226 za mbegu za bangi zilikamatwa, huku mkoani Tabora kilogramu 4,650.86 za bangi pamoja na kilogramu 203 za mbegu za bangi zilikamatwa. “Kwa upande wa mirungi, operesheni zimebaini matumizi ya pikipiki na mabasi ya abiria katika usafirishaji wa dawa hiyo, hususan katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Dodoma, ambapo jumla ya kilogramu 6,412.89 za mirungi zilikamatwa,amesema. Kamishina Jenerali Lyimo amesema katika moja ya matukio hayo, watuhumiwa watatu walikamatwa wakisafirisha bunda 238 za mirungi zenye uzito wa kilogramu 125.33 kwa kutumia basi la kampuni ya RATCO, lenye namba za usajili T.443 EMG, ililokuwa likifanya safari kati ya Tanga na Dar es Salaam. Aidha, mkoani Tabora, Wilaya ya Uyui, kilogramu 21.95 za bangi zilikamatwa katika gari aina ya TATA lenye namba za usajili T.381 DWU, lililokuwa likifanya safari kati ya Uyui mkoani Tabora na Kahama. Watuhumiwa watano walikamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Tue, 29 Sep 2026 15:34:49 +0000
Uncategorized · SoftPower News

Uganda Coffee Prices Ease as Global Robusta, Arabica Markets Decline

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Aliko Dangote dismisses Lamu refinery court dispute as ‘normal’ for African projects

Business · 5 hours ago

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

RAIS MWINYI ATAKA MAONESHO YA TECH NA AI YALETE MATOKEO KWA WANANCHI, YAS KUENDELEA KUWEKEZA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka washiriki wa Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia na Akili Unde (Tech & AI International Expo 2026) kuyageuza majadiliano kuwa ushirikiano wenye matokeo kwa wananchi. Katika maonesho hayo, Yas Tanzania imesema itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya mawasiliano na kuchochea huduma za kidigitali visiwani Zanzibar. Akifungua maonesho hayo leo katika hoteli ya Golden Tulip Zanzibar, Dkt. Mwinyi alisema teknolojia ina mchango mkubwa katika kuboresha huduma za afya, elimu na huduma za umma, pamoja na kufungua fursa za biashara na ajira. “Maonesho haya yanatoa nafasi muhimu ya kubadilishana mawazo, kujenga ushirikiano, kuonesha ubunifu na kutafakari namna teknolojia inavyoweza kuchochea maendeleo yanayomfikia kila mmoja na kuijenga kesho yetu,” alisema. Rais Mwinyi aliwataka wabunifu kutafuta suluhisho kwa changamoto zinazowakabili wananchi. Alisema manufaa ya teknolojia yanapaswa kuwafikia pia wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na wakazi wa maeneo ya pembezoni ambao hawajafikiwa na huduma. Kwa upande wake, Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu Zanzibar, Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga, alisema vijana wanahitaji mazingira yatakayowawezesha kutumia ujuzi wa kidijitali kuanzisha biashara na kuhudumia wateja ndani na nje ya Zanzibar. “Kijana wa Zanzibar anahitaji tu kuwa na wazo, kitendea kazi na huduma ya intaneti, kisha kujenga biashara inayohudumia wateja hapa nchini na hata nje ya mipaka yetu,” alisema. Soraga alisema Serikali inaweka sera na kanuni zitakazosaidia kampuni changa za teknolojia kukuza biashara zao. Naye, Ofisa Mkuu wa Biashara wa Yas Tanzania, Bw. Norman Kiondo, alisema kampuni hiyo itaendelea kuwekeza katika mtandao na kushirikiana na wadau kufikisha huduma za kidijitali kwa wananchi na biashara nyingi zaidi. Alisema kwa hapa Zanzibar, Yas inashirikiana na ZICTIA kupanua huduma za intaneti ya (faiba) kuchochea huduma ya intaneti majumbani, taasisi na biashara Zanzibar ambapo imewekeza zaidi ya Sh bilioni 300. Kwa mujibu wa Kiondo, Yas vilevile, imewekeza zaidi ya Sh trilioni 1.2 katika mtandao wake nchini, na sasa ina zaidi ya minara 4,900 na zaidi ya kilomita 5,700 za miundombinu ya intaneti ya faiba. Alisema mawasiliano bora Zanzibar yatawezesha biashara za utalii kuwahudumia wageni, wajasiriamali kuwafikia wateja na taasisi za umma kutoa huduma kwa urahisi zaidi. “Tutaendelea kuwekeza na kuboresha miundombinu yetu ya mawasiliano ili kuwa na mtandao imara hapa Zanzibar. Pia tutaendelea kushirikiana na Serikali na taasisi mbalimbali kusaidia biashara kutumia teknolojia na kuchochea ubunifu,” alisema Kiondo

Tue, 29 Sep 2026 09:00:00 +0000
Uncategorized · SoftPower News

Museveni Salutes King Oyo, Says He Was Saddened to Find His June 15 Letter After Burial

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Kwetu eSIM launches on Safaricom’s M-Pesa Super App

Latest · Business

Recently

Page 976 of 1126 · 22511 stories