Search the region
22511 stories
MIGIRO AFUNGUA SEMINA ELEKEZI KWA KAIMU MAKATIBU WA CCM MIKOA 32
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Asha-Rose Migiro, amefungua semina elekezi kwa Kaimu Makatibu wa CCM Mikoa 32, leo Septemba 29, 2026, jijini Dodoma. Semina hiyo ya siku mbili inalenga kuwajengea uwezo viongozi hao kuhusu majukumu yao ya kiuongozi, uendeshaji wa shughuli za chama pamoja na utekelezaji wa mipango na maelekezo ya Chama Cha Mapinduzi. Akifungua semina hiyo, Ndugu Migiro amesisitiza umuhimu wa viongozi hao kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, weledi na kuzingatia misingi, kanuni na taratibu za chama.
Tue, 29 Sep 2026 13:50:07 +0000Four convicted over 2015 murder of former MP George Muchai
Read the full report from the original source.
RecentlyCopia Kenya investors face big losses as startup goes into liquidation
Read the full report from the original source.
RecentlyUK PM Burnham seeks 'hope again' at Labour Party conference
Read the full report from the original source.
RecentlyRights group takes case of 95-year-old detained Korean religious leader to UN
A Paris-based rights organisation has asked the United Nations Human Rights Council to press the Republic of Korea to find an alternative to pretrial detention for a 95-year-old religious leader. CAP...
RecentlyInside the Ksh.2 trillion Dangote Oil refinery in Lamu
Read the full report from the original source.
RecentlySafaricom, M-Pesa Foundations fete inaugural Capture the Good winners
Business · 3 hours ago
RecentlyDangote says refinery IPO will democratise wealth creation
Africa · 3 hours ago
RecentlyHousekeeper tells court Cohen cried ‘you are killing me’ during alleged 2019 assault by Sarah
Latest · News
RecentlyStripped titles? How Man City cheating scandal could play out
Charges cover several areas, including the accuracy of financial information supplied to the Premier League.
RecentlyMBT yavuta umati Geita, Wizara ya Madini yafungua dirisha jipya la fursa kwa vjana na waawake
Read the full report from the original source.
RecentlyDar braces for Power & Energy Tanzania Expok
DAR ES SALAAM: THE 10th Power & Energy Tanzania 2026 and the 10th Solarexpo Tanzania 2026 is expected to take…
RecentlyUtekelezaji Usio Sawa wa Kanuni za Usafiri Mtandao Wazua Wasiwasi wa Usalama na Ushindani
Uchunguzi uliofanywa katika sekta ya usafiri wa mtandao nchini Tanzania umeibua wasiwasi kwamba kutokuwapo kwa usawa katika utekelezaji wa masharti ya udhibiti kunahatarisha usalama wa abiria, huku kukiziweka katika mazingira magumu kampuni zinazowekeza fedha nyingi kutimiza matakwa ya kisheria. Waandishi wa habari waliojaribu taratibu za usajili walibaini kuwa baadhi ya makampuni yaliwaruhusu madereva wanaotaka kujiunga kuendelea na mchakato bila kuwasilisha kikamilifu nyaraka muhimu, ikiwemo picha, leseni sahihi ya udereva, kadi ya usajili wa chombo, leseni ya LATRA na nyaraka za bima. Majaribio ya usajili yaliyofanywa kwa kificho yalibaini tofauti kubwa katika masharti ya kuwapokea na kuwahakiki madereva kati ya kampuni moja na jingine. Hali hiyo imeongeza wasiwasi miongoni mwa baadhi ya wadau kwamba waendeshaji wanaokabiliwa na uangalizi mdogo wa udhibiti wanalegeza masharti ya uhakiki ili kuongeza idadi ya madereva kwa kasi. Mbinu hiyo inaweza kuharakisha uongezekaji wa madereva kwenye aplikesheni, lakini pia inatengeneza mazingira yasiyo sawa kibiashara. Kampuni zinazolipia leseni, uhakiki wa madereva, bima, mifumo ya uzingatiaji wa kanuni na kodi hubeba gharama ambazo washindani wasiotimiza masharti kikamilifu huziepuka. Matokeo yake ni kuwapo kwa faida isiyo ya haki katika gharama za uendeshaji, hali inayoweza kuvuruga ushindani wa nauli na kukatisha tamaa uwekezaji wa muda mrefu katika sekta hiyo. Athari zake kwa usalama nazo ni kubwa. Baadhi ya abiria waliohojiwa walisema wamekutana na akaunti zisizo na picha za madereva, majina yanayoonekana kuwa ya utani badala ya utambulisho unaoweza kuthibitishwa, pamoja na magari yanayofika yakiwa na taarifa tofauti na zile zilizooneshwa kwenye programu. Kanuni za LATRA zinataka magari ya kukodi kuwa na leseni halali, huku waendeshaji wa makampuni ya taxi mtandao wakitakiwa kuhakikisha madereva na magari yanayosajiliwa yanakidhi viwango vilivyowekwa. Matokeo ya uchunguzi huo yanaimarisha hoja ya kuitaka LATRA kusimamia masharti ya uzingatiaji wa sheria kwa usawa katika makampuni ya taxi mtandao yote. Ushindani wa haki hauwezi kuwepo ikiwa baadhi ya waendeshaji wanabeba gharama kamili za udhibiti huku wengine wakikua kwa kukwepa masharti hayo. Utekelezaji wenye usawa ni muhimu katika kulinda abiria, kuhifadhi imani ya wawekezaji na kujenga sekta endelevu ya usafiri wa kidijitali nchini Tanzania.
Tue, 29 Sep 2026 13:38:56 +0000WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUZINGATIA VIAPO
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza leo tarehe 29 Septemba 2026 mkoani Tabora wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na Kata 11 za Tanzania bara. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza leo tarehe 29 Septemba 2026 mkoani Tabora wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na Kata 11 za Tanzania bara. Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima akizungumza jambo wakati wa mafunzo hayo. Sehemu ya wajumbe wa Management ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma na Kata 11za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ****** Na. Mwandishi Wetu, Tabora Watendaji wa uchaguzi wamesisitizwa kuheshimu viapo vyao na kutekeleza majukumu kwa kuzingatia Katiba, sheria na kanuni wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao. Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele leo tarehe 29 Septemba, 2026 mkoani Tabora wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi. Mafunzo hayo ni sehemu ya mchakato wa maandalizi ya uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye Jimbo la Chamwino Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma na Kata 11 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 04 Novemba, 2026. “Ninawasisitiza kuheshimu viapo vyenu kwa nafasi mlizoteuliwa, tekelezeni majukumu yenu kwa kuzingatia Katiba ya Nchi, sheria za uchaguzi na kanuni zake, kanuni za maadili ya uchaguzi na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na yatakayotolewa na Tume katika kipindi hiki cha uchaguzi,” amesema Jaji Mwambegele. Amewaelekeza watendaji hao kuhakikisha kuwa wakati wote wa mchakato wa uchaguzi huo, wanavishirikisha kwa karibu vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili na wadau wengine wa uchaguzi katika maeneo yao kuhusu masuala ya kiuchaguzi ambayo wanastahili kushirikishwa. Ameongeza kuwa watendaji hao wanapaswa kuvipatia vyama vya siasa orodha ya vituo vya kupigia kura ili kuviwezesha kupanga mawakala. “Ni muhimu kwenu pia, kuhakikisha mnayatambua na kuyajua vyema maeneo ambayo uchaguzi utaendeshwa ikiwemo miundombinu ya kufika katika vituo vya kupigia kura,” amesema Jaji Mwambegele. Amewaasa watendaji hao kuhakikisha kuwa pamoja na uzoefu ambao baadhi yao wanao katika uendeshaji wa uchaguzi, wanaepuka kufanya kazi kwa mazoea kwa kuwa kila uchaguzi unatofautiana na uchaguzi mwingine. Jaji Mwambegele amewasisitiza watendaji hao kuhakikisha wanaajiri watendaji wa vituo wenye sifa, weledi, wanaojitambua na kuachana na upendeleo kwa ndugu na jamaa ambao hawana sifa za kufanya shughuli za uchaguzi. “Mhakiki vifaa vya uchaguzi mnavyopokea kutoka Tume na kuhakikisha kila mkuu wa kituo anapata vifaa vyote vya uchaguzi vinavyohitajika mapema na kuhakikisha siku ya uchaguzi mnaweka utaratibu utakaowezesha kila kituo cha kupigia kura kufunguliwa saa 1:00 asubuhi,” amesema. Mafunzo hayo ya siku tatu yanawajumuisha waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na kata, maafisa uchaguzi, maafisa ununuzi na wahasibu. Kata 11 za Tanzania Bara zitakazofanya uchaguzi wa Udiwani ni Nonde iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya; Lugenge, Halmashauri ya Mji Njombe; Bargish, Halmashauri ya Mji Mbulu; Makole, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza; Mwera, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Oldonyosambu, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro. Nyingine ni Igalula iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Uyui; Shelui, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba; Mvumi, Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa; Nyarero, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na Ilolangulu, Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe. Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma na Kata 11za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma na Kata 11za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. Naibu Msajili na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Tabora Mhe. Gabriel Patrick Ngaeje akiwaongoza washiriki wa mafunzo kula kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa pamoja na kutunza siri wakati wakitekeleza majukumu ya Uchaguzi. Washiriki wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kutunza siri.
Tue, 29 Sep 2026 13:31:46 +0000TTCL YAAHIDI KUENDELEA KUSIMAMIA MIUNDOMBINU IMARA YA MAWASILIANO NCHINI
Na MWANDISHI WETU - ARUSHA Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuimarisha nafasi yake katika kuwezesha shughuli za Serikali kidijitali kwa kutoa huduma ya intaneti yenye uhakika na kuwekeza katika miundombinu ya mawasiliano inayosaidia utekelezaji wa shughuli za Serikali, taasisi na mashirika ya umma nchini. TTCL imetoa huduma hiyo katika Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (Chairpersons and CEOs Forum), kinachofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), ambapo huduma ya intaneti imewawezesha washiriki kupata na kubadilishana taarifa kwa wakati, kufanya mawasiliano ya kidijitali na kutumia mifumo mbalimbali katika shughuli za kikao. Kikao hicho cha siku tatu kimefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndenjembi, kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kinawakutanisha Wenyeviti wa Bodi, Wakuu wa Taasisi pamoja na viongozi mbalimbali kujadili masuala ya kimkakati yanayohusu uongozi, uwajibikaji, utawala bora na uboreshaji wa utendaji wa taasisi na mashirika ya umma. Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufunguliwa kwa kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Moremi Marwa, amesema Shirika hilo litaendelea kuwezesha uchumi wa kidijitali kupitia uwekezaji na usimamizi wa miundombinu ya mawasiliano, huduma za kifedha za kidijitali na teknolojia zinazochochea maendeleo ya taifa. Bw. Marwa amesema miundombinu ya mawasiliano ina nafasi muhimu katika kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hususan katika kukuza uchumi wa kidijitali na kuwawezesha wananchi, wafanyabiashara na taasisi kupata huduma kwa kutumia teknolojia za kisasa. Ameeleza kuwa TTCL inaendelea kuwekeza na kusimamia miundombinu ikiwemo Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, minara ya mawasiliano na Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data (National ICT Data Centre), ambayo inawezesha upatikanaji wa mawasiliano, uhifadhi wa taarifa na matumizi ya huduma mbalimbali za kidijitali. Kwa mujibu wa Bw. Marwa, jukumu la TTCL ni kuhakikisha miundombinu hiyo inaendelea kujengwa, kuimarishwa na kusimamiwa kwa ufanisi ili huduma za mawasiliano zipatikane kwa uhakika na kusaidia shughuli za kiuchumi katika maeneo mbalimbali nchini. Aidha, amesema TTCL inachangia kuwezesha miamala ya kifedha ya kidijitali kupitia huduma zake, huku ikiendelea kuunga mkono juhudi za kukuza ajira kwa vijana kupitia programu za mafunzo kwa vitendo na kuwashirikisha katika shughuli za mawasiliano ya simu pamoja na usambazaji wa huduma za intaneti kwa teknolojia ya faiba kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Akizungumzia matumizi ya Akili Unde (Artificial Intelligence – AI), Bw. Marwa amesema teknolojia hiyo inahitaji miundombinu imara ya mawasiliano pamoja na uwezo wa kutosha wa kuhifadhi na kuchakata data. Amesema TTCL inaendelea kuboresha na kupanua uwezo wa Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya huduma za kidijitali na teknolojia mpya. Utoaji wa huduma ya intaneti katika kikao hicho unaakisi dhamira ya TTCL ya kuendelea kuwa mhimili wa mawasiliano nchini kwa kuiwezesha Serikali, taasisi na mashirika ya umma kupata miundombinu na huduma za mawasiliano zinazochochea ufanisi katika utendaji, ushirikiano na utoaji wa huduma kwa wananchi. Kupitia uwekezaji katika miundombinu na uboreshaji wa huduma za mawasiliano, TTCL inaendelea kuchangia utekelezaji wa ajenda ya Mageuzi ya Kidijitali Tanzania kwa kuhakikisha teknolojia inatumika kuongeza tija, uwajibikaji na ufanisi katika shughuli za Serikali na uchumi kwa ujumla.
Tue, 29 Sep 2026 13:35:42 +0000Jambojet suspends Zanzibar flights
Read the full report from the original source.
RecentlyTanzania calls on AIIB to cement ties with its members in supporting infrastructure development
DOHA: THE Minister for Finance, Khamis Mussa Omar, has called on the Asian Infrastructure Investment Bank (AIIB) to strengthen cooperation…
RecentlyTanzania yafungua milango wawekezaji Finland
Read the full report from the original source.
RecentlyJambojet stops Zanzibar flights as fuel, insurance costs bite
Read the full report from the original source.
RecentlyCounties, public universities lead in Sh3.92bn unremitted Sacco deductions
Business · 4 hours ago
RecentlyPage 979 of 1126 · 22511 stories