Search the region
22505 stories
61 suspected gang members arrested in Kitale crackdown
Read the full report from the original source.
RecentlyWhat US diesel export ban could mean for you The US is one of the world's leading energy producers
The US is one of the world's leading energy producers
RecentlyUn Nigérian tente de battre le record du monde en dansant sans interruption pendant sept jours
Des foules se sont rassemblées à Lagos pour regarder Ben Dancer, qui affirme qu'il continuera à danser jusqu'à mercredi matin.
RecentlyCaptain Morgan Joins 6th Edition of Qweshunga Day for Nostalgic Party & Play
Read the full report from the original source.
RecentlyUganda Embassy in Copenhagen Leads MDAs into Strategic Cooperation In Infrastructure, Health and Emergency Services
Read the full report from the original source.
RecentlyHackers Are Hijacking Cloud Accounts to Run AI Models on Someone Else’s Bill
Read the full report from the original source.
RecentlyPolice reveal Cohen, Wairimu's repeated disputes before murder
Police told the High Court that domestic disputes between slain Dutch businessman Tob Cohen and his wife Sarah Wairimu had drawn police attention months before his death.
Mon, 28 Sep 2026 21:09:00 +0300Deux fusillades endeuillent l'Afrique du Sud
Read the full report from the original source.
RecentlyTruecaller says Nigerians can remove their numbers after privacy ruling
Read the full report from the original source.
RecentlyThree testify as Cohen murder trial continues The case will continue on September 29, 2026, when the prosecution is expected to call additional witnesses.
The case will continue on September 29, 2026, when the prosecution is expected to call additional witnesses.
RecentlyCourt orders status quo on Manda Magogoni and as residents challenge takeover
Read the full report from the original source.
RecentlyRate of growth of regulated Saccos total assets in Kenya Amounts in Ksh billions
Amounts in Ksh billions
RecentlyDj Phaphane to Bring Cancun Energy to Mediterraneo this Sunday
Read the full report from the original source.
RecentlyMan dances non-stop for 7 days in world record bid The Guinness World Records has yet to confirm whether the attempt qualifies as an official record.
The Guinness World Records has yet to confirm whether the attempt qualifies as an official record.
RecentlyJamii Yahimizwa Kupima Seli Mundu Kabla ya Ndoa
Dkt. Yonazi Charles, Mkurugenzi Mtendaji wa Masaki Wellspring Hub, ambao ni waandaaji wa Masaki Health Expo ( wa nne kushoto mwenye miwani) pamoja na wadau wengine wakimsikiliza Dr.Living Dennis Nyaki katika maonesho hayo yaliyofanyika Masaki, jijini Dar es Salaam. Mmoja wa wananchi akichangia damu wakati wa maonesho ya Afya ya Masaki ( Masaki Health Expo 2026) katika jitihada za kupambana na ugonjwa wa Seli Mun Na Mwandishi Wetu JAMII imetakiwa kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara, ikiwemo kupima ugonjwa wa seli mundu (sickle cell), huku vijana wakihimizwa kupima vinasaba vya ugonjwa huo kabla ya kuingia kwenye ndoa ili kupunguza uwezekano wa kupata watoto wanaozaliwa na ugonjwa huo. Akizungumza jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa matembezi na maonesho yaliyolenga kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa seli mundu, Mratibu wa Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza mkoani humo, Dkt. Living Dennis Nyaki, amesema seli mundu ni ugonjwa wa kurithi unaoweza kumpata mtoto pale wazazi wote wawili wanapokuwa na vinasaba vinavyosababisha ugonjwa huo. Dkt. Nyaki amesema vijana wanapaswa kupima na kufahamu hali zao za vinasaba kabla ya kuingia kwenye ndoa, ili waweze kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya na uzazi. Pia amesisitiza umuhimu wa kuwapeleka watoto kupima ili kutambua hali zao mapema na kuwawezesha kupata huduma stahiki. “Ni muhimu vijana kupima kabla ya kuingia kwenye ndoa ili kujua kama wana vinasaba vya seli mundu. Hii itasaidia kuongeza uelewa na kuchukua hatua sahihi za kiafya kabla ya kupata watoto,” amesema. Aidha, Dkt. Nyaki ameitaka jamii kubadili mfumo wa maisha ili kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa kufanya mazoezi mara kwa mara, kuzingatia ulaji salama na kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Masaki Wellspring Hub, Dkt. Yonazi Charles Senkondo, ambao ni waandaaji wa matembezi na maonesho hayo kwa kushirikiana na Ruge Mutahaba Foundation, amesema shughuli hiyo imelenga kuhamasisha jamii kuwa na uelewa kuhusu seli mundu na umuhimu wa kupima, sambamba na kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi na ugonjwa huo. Naye Dkt. RhobiJeremiah Zakaria kutoka Ruge Mutahaba Foundation amesema inakadiriwa kuwa kati ya watoto 11,000 na 14,000 huzaliwa kila mwaka wakiwa na ugonjwa wa seli mundu, akisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za mapema kupitia elimu na upimaji. Katika kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kupima, Balozi wa Seli Mundu na Miss Universe Tanzania 2026, Queen Elizabeth, amesema kuwa yeye anaishi na changamoto hiyo na ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kupima afya na kufahamu hali zao za vinasaba kabla ya kuingia kwenye mahusiano na ndoa. “Mimi ni mama wa mtoto mwenye changamoto hiyo, hivyo ni ugonjwa ambao nimekuwa nikiishi nao. Naiasa jamii kuwa na utamaduni wa kupima afya na kujua vinasaba vyetu tunapokutana na wenza wetu. Ni muhimu kupima,” amesema. Queen Elizabeth amesema ugonjwa wa seli mundu unaweza kuwa na gharama kubwa za matibabu, akieleza kuwa baadhi ya matibabu yanaweza kugharimu kiasi kikubwa ambacho familia nyingi haziwezi kumudu. Amesema Serikali inatoa huduma ya upandikizaji wa uboho katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, lakini gharama ya huduma hiyo, inayokadiriwa kufikia takribani Sh milioni 75, bado ni changamoto kwa watu wengi, huku akieleza kuwa ni watu wachache tu wameweza kupata huduma hiyo hadi sasa. “Katika uhalisia wa maisha ya kawaida, kwa Watanzania zaidi ya milioni 60, watu wengi hawawezi kumudu gharama hizi. Hivyo ni muhimu kupima mapema ili ujue kama unabeba kinasaba na kuchukua hatua ili kuzuia mtoto kuzaliwa akiwa na ugonjwa huo,” amesema. Queen Elizabeth ameipongeza Masaki Wellspring Hub kwa kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchukua hatua za mapema dhidi ya seli mundu, huku akiwataka Watanzania kuendelea kupima afya zao na kuchukua hatua stahiki. Hii ni mara ya tatu kwa Masaki Wellspring Hub kuandaa uko hilo ili kuongeza uelewa , kuima na kutoa ushauri juu ya magonjwa yasiyoambukiza Wadau waliounga mkono tukio hilo mwaka huu ni pamoja na Kanisa la Waadventista wa Sabato Masaki, Elveth Group, Choplife Foundation na Fortune Management Consulting.
Mon, 28 Sep 2026 17:34:27 +0000TANZANIA KUWA MWENYEJI WA DOHA DIALOGUE AFRIKA
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, utakaofanyika Oktoba 5 na 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam, ukiwa ni mkutano wa kwanza kufanyika ndani ya bara la Afrika. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Deus Sangu, alisema kuwa mkutano huo utatoa fursa kwa Tanzania kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika na GCC+ katika masuala ya uhamaji wa nguvu kazi na ajira. Mkutano huo utawakutanisha nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, Baraza la Ushirikiano wa Nchi za Ghuba (GCC+), ambazo ni Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar, Kuwait, Oman na Bahrain, pamoja na Jordan na Lebanon. Sangu alisema mkutano huo ni jukwaa la kimataifa linalolenga kuimarisha ushirikiano katika usimamizi wa uhamaji wa nguvu kazi na kukuza ajira zenye staha, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. “Na katika mkutano huu mkuu kabisa, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassan,” alisema. Alisema Mkutano wa Kwanza wa Doha Dialogue ulifanyika jijini Doha, Qatar, Mei 21 na 22, 2024, ukihusisha nchi 33, ikiwemo nchi 25 za Afrika, nchi za Ghuba pamoja na Jordan na Lebanon, huku Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zilizoshiriki. Kwa mujibu wa Sangu, mkutano huo ulipitisha azimio lililoitwa Doha Declaration, lililoweka msingi wa kuendeleza majadiliano na ushirikiano kati ya nchi za Afrika na nchi za Kiarabu kuhusu uhamaji wa nguvu kazi. “Tanzania ni nchi ya pili kuwa mwenyeji wa Doha Dialogue, mkutano huu ambao unafanyika kila baada ya miaka miwili. Na kwa mara ya kwanza ndio unafanyika ndani ya bara la Afrika,” alisema. Alisema maeneo muhimu yatakayojadiliwa ni pamoja na uimarishaji wa mikataba ya ajira baina ya nchi, uoanishaji wa ujuzi wa wafanyakazi na mahitaji ya soko la ajira na ujenzi wa mifumo ya uhamaji wa nguvu kazi inayoweza kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia, mahitaji mapya ya soko la ajira na kazi zenye staha. Sangu alisema mkutano huo pia utatoa fursa kwa Tanzania kuimarisha nafasi yake katika mijadala ya kimataifa kuhusu uhamaji wa nguvu kazi, kupanua fursa za ajira nje ya nchi, kulinda haki za wafanyakazi na kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika na GCC+. “Mkutano huu pia utaongeza ushindani wa nguvu kazi ya Tanzania na kuchangia katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050,” alisema. Alisema Serikali itaendelea kutoa elimu kupitia balozi pamoja na kuwa na siku maalum za kukutana na Watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi ili kupata mrejesho kuhusu mazingira yao ya kazi.
Mon, 28 Sep 2026 17:29:23 +0000Museveni Bids Farewell to Outgoing Indian High Commissioner
Read the full report from the original source.
RecentlySERIKALI KUONGEZA FEDHA UZAZI WA MPANGO
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv SERIKALI imeahidi kuongeza fedha za ndani kwa ajili ya bidhaa za uzazi wa mpango kwa angalau asilimia 10 kila mwaka, ikiwa ni hatua ya kuimarisha huduma za afya ya uzazi na kuchangia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050. Ahadi hiyo ilitolewa Septemba 28,2026 jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uzazi wa Mpango Duniani na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga katika Wizara ya Afya, Ziada Sellah, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Grace Magembe. Sellah alisema uzazi wa mpango ni uwekezaji muhimu katika afya ya watu, ustawi wa familia na maendeleo ya Taifa, kwa kuwa unaziwezesha familia kufanya maamuzi kuhusu idadi ya watoto na muda wa kupanga kati ya uzazi mmoja na mwingine. “Ahadi ya Tanzania ya Uzazi wa Mpango 2030 inatoa msingi muhimu wa kuimarisha ufadhili endelevu wa ndani wa uzazi wa mpango, ikiwa ni pamoja na kuongeza rasilimali za ndani kwa ajili ya bidhaa za uzazi wa mpango kwa angalau asilimia 10 kila mwaka na kuhakikisha fedha zilizotengwa zinatolewa kikamilifu,” alisema. Alisema kuongeza uwekezaji katika uzazi wa mpango kutasaidia pia kuharakisha utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, hususan Lengo la Tatu linalohusu afya bora na ustawi. Naibu Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Melissa McNeil-Barrett, alisema uzazi wa mpango haupaswi kuangaliwa kwa upande wa upatikanaji wa bidhaa na huduma pekee, bali pia kuhakikisha watu wanapata taarifa sahihi na wanaweza kufanya maamuzi yenye uelewa kuhusu afya yao ya uzazi. “Uzazi wa mpango hauhusu tu upatikanaji wa bidhaa na huduma. Pia ni kuhakikisha watu wanapata taarifa sahihi, wanaweza kupata huduma hizo na wako huru kufanya maamuzi yenye uelewa kuhusu afya yao ya uzazi,” alisema. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa MSI Tanzania, Patrick Kinemo, alisema mabadiliko katika ufadhili kutoka kwa wafadhili yameongeza umuhimu wa Serikali kuimarisha uongozi, ushirikiano na umiliki wa kitaifa katika kuhakikisha huduma hizo zinaendelea kupatikana. Alisema uzazi wa mpango ni sehemu muhimu ya afya ya mama, mtoto mchanga na afya ya uzazi, huku akibainisha kuwa huduma hizo za hiari zinaweza kuchangia ujauzito wenye afya na kupunguza vifo vya akina mama vinavyoweza kuzuilika. Kinemo alisema bado kuna vikwazo vinavyoathiri upatikanaji wa huduma hizo, ikiwamo ukosefu wa taarifa, taarifa potofu, changamoto za kifedha na kijiografia pamoja na vikwazo vya kijamii na ndani ya mfumo wa afya. Alisema washirika wanaendelea kushirikiana na Serikali kusogeza huduma karibu na jamii, hususan maeneo ya pembezoni, pamoja na kujenga uwezo wa wahudumu wa afya na kuboresha ubora na upatikanaji wa huduma. Kaulimbiu ya mwaka huu ya “Hakuna Vikwazo, Chaguo Pekee” inalenga kuhimiza upatikanaji wa taarifa sahihi, huduma bora na chaguo mbalimbali za uzazi wa mpango kwa wanawake, wasichana, vijana, wanandoa na watu binafsi. Siku ya Uzazi wa Mpango huadhimishwa duniani kote Septemba 26 kila mwaka kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu uzazi wa mpango na kuwawezesha watu kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya yao ya uzazi.
Mon, 28 Sep 2026 17:24:28 +0000« Je suis née alors que ma mère était maintenue en vie dans un poumon d'acier »
La mère de Susan, Elizabeth, était enceinte de cinq mois lorsqu'elle a contracté la polio dans les années 1950.
RecentlySerikali Yaimarisha Ulinzi na Ustawi wa Watu wenye Ualbino
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 999 of 1126 · 22505 stories